Header Ads Widget

WAZIRI WA ELIMU Z'BAR AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA WA SENSA TANZANIA

 


WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Simai Mohammed Said amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Sensa Tanzania Balozi Mohammed Haji Hamza ofisini kwake Mazizini Mjini Unguja.


Katika mazungumzo yao Balozi Hamza amemuomba Mhe. Simai kumpa mashirikiano wakati wa Zoezi la sensa litakapofanyika hasa kwa upande wa walimu kwani wao ndio waelimishaji wazuri katika jamii.


Amesema wana kazi kubwa ya kuelimisha jamii ambapo Wizara ya Elimu ndio inahusika na suala hilo kutokana na kuwa na utaratibu mzuri wa kuwasomesha Wanafunzi  ili nao wawaelimishe wazazi wao juu ya suala zima la sensa.


Aidha amefahamisha kuwa wameandaa zoezi la utungaji wa Insha itakayokuwa na ushindani wa Kimkoa ambayo itawahusisha Wanafunzi wa Sekondari, hivyo amemuomba Mhe. Waziri utakapofika muda kuwaruhusu Wanafunzi ikiwa ni miongoni mwa kuhamasisha jamii kushiriki zoezi hilo la sensa.


Hata hivyo Balozi Hamza amesema hivi sasa utaratibu wa zoezi hilo unaendelea vizuri kwa kufanyika zoezi la kukata mitaa pamoja na kuweka majina katika maeneo mbalimbali nchini,  pamoja na kukamilisha zoezi la anuani za posta na makaazi ambalo lilikuwa halijakamilika. 


Amesema sensa ya mara hii itakuwa ni tifauti na sensa zilizopita kutokana na wakati ulivyi sasa pamoja na mifumo ya kisasa itakayotumika katika kuendesha zoezi hilo.



Nae Mhe Simai amemuahidi Balozi Hamza kuwa Wizara itatia ushirikiano huo kwa Kuwaruhusu Walimu wake huku akimtaka kutoa taarifa wakati utkpofika ili ziweze kufika kwa Skuli husika.


Amesema Walimu ni watu muhimu na wanakubalika sana na jamii na hivyo wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo katika nchi.


Aidha Mhe. Simai amesema kutokana na umuhimu wa Sensa duniani kote, kuna haja ya kuwatumia Viongozi  wa dini, watu maarufu waliokubalika katika jamii pamoja na wanasiasa katika kufikisha ujumbe ili jamii iweze kuhamasika kwa haraka na kuweza kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo litakapofika ili malengo yaliyopangwa na Serikali yaweze kufikia.


Zoezi la Sensa ya sita tokea kupata uhuru inatarajiwa kufanyika mwezi 8-2022  ambapo itahusisha sensa ya watu na makaazi pamoja na sensa ya majengo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI