Header Ads Widget

VIJANA WAJASIRIAMALI NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA KUZALISH BIDHAA ZENYE UBORA

 


WAJASIRIAMALI Hususani Vijana Nchini wametakiwa kuwa wabunifu na kuzalisha Bidhaa zenye ubora zitakazoweza kuhimili Ushindani wa Soko la Biashara.


Wito huo umetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Masoud Othaman katika hafla ya kukabidhi ruzuku za fedha kwa vikundi 15 vya vijana wajasiriamali kutoka Bara na Zanzibar huko katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Marekani la USAID. 


Amesema ni vyema Wajasiriamali kuwa wabunifu wakati za Uzalishaji wa Bidhaa ili kuzalisha bidhaa zenye ubora unahitajika katika Soko la Biashara Nchini.


Pia amewataka Wajasiriamali Vijana kuhakikisha wanatumia vizuri fedha walizopewa kwa malengo yaliyokusudiwa.



“Ni vyema sasa mukahakikisha fedha hizi mulizopatiwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuzalisha Bidhaa mbalimbali kupitia vikudi vyenu,”aliesema.


Aliongeza kuwa, Matarajio kuwa Fedha hizo zitatumika ipasavyo kwa kuwainua kiuchumi na kuzaa matokeo chanya.


“Fedha hizi Dola Milioni Moja zilizotolewa kwa vikundi hivi kupitia Mradi wa Inua Vijana, iwapo zitatumika ipasavyo na kwa malengo yaliyokusudiwa zitaweza kutoa matokeo mazuri ya kimaendeleo kwa vijana nchini,”alieleza.







Hata hivyo Makamu wa Kwanza wa Rais  amesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua na kuthamini ipasavyo mchango wa maendeleo unaotolewa na serikali ya  Watu wa Marekani  ambao unachangia sana katika kuleta ustawi wa jamii katika maeneo na sekta mbali mbali za kimaendeo hapa Zanzibar.


Katika Hatua nyingine Makamu wa Kwanza wa Rais ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kutunza amani iliyopo ambayo imepatikana kwa gharama kubwa ya umoja, mshikamano  na maridhiano ya kisiasa ambayo aliomba kutunzwa kwa ajili ya msuatakabili mwema wa Zanzibar.


Nae Waziri wa Uchumi wa Bluu Zanzibar Mhe. Abdalla Hussein Kombo amewataka vijana kuutumia vyema msaada huo ili kuimarisha maendeleo na kusaidia kuimarisha maendeleo.


Mapema Mkurugenzi Mkaazi wa shirika la Msaada la Watu wa Marekani USAID, Kate Somvongsiri amesema kwamba Zanzibar inafursa kubwa za kuweza kuwasaidia vijana kupata ajira na kwamba shirika hilo litaendelea kusaidia katika jitihada za kuleta maendeleo ya vijana na jamii kwa jumla.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI