Waziri wa nchi ofisi ya Rais,Utawala Bora , Mohamed Mchengerwa amewataka Wananchi na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) kuhoji matumizi ya mamilion ya fedha yaliyopelekwa katika maeneo yao kupitia na serikali kupitia Mfuko wa TASAF .
Akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Oldonyowasi wilayani Arumeru,Leo 13,Novemba 2021, wakati Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na serikali za mitaa ilipotembelea Kijiji hicho amesema serikali ya Rais Samia Suluhu imetoa fedha katika halmashauri zote nchini hivyo Wananchi wasisite kutumia haki yao kwenda ofisi za halmashauri kuwauliza wakurugenzi matumizi ya fedha.
" Tunataka Takukuru
kufatilia matumizi ya fedha hizi na Wananchi tukieni haki yenu ya kupata habari nendeni katika halmashauri waulizeni wakurugenzi , thamani ya miradi wanavyotekeleza kwenye ujenzi wa miundombinu,huduma za afya na nyingine"amesema
Alisema Rais Samia Suluhu ameongeza fedha katika halmashauri zote nchini kuhakikisha Taifa linapambana na umasikini, kujenga shule ,vituo vya Afya na miradi kadhaa ya miundombinu mbinu.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema Mfuko huo upo katika utekelezwaji wa miradi ya awamu ya nne imetoa milioni 130 mikoa ambayo itanufaika ni Arusha,Geita,Simiyu,Mwanza na Njombe.
" Tunataka miradi yote itekelezwe kwa uadilifu na kwa wakati katika Maeneo ambayo yatapata fedha" amesema
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Sebastian Kapufi amewataka Wananchi kuhakikisha wanaitunza miradi ambayo inafadhiliwa na TASAF.
Amesema wameridhika na miradi katika Kijiji hicho ambapo TASAF imejenga madarasa,jengo la utawala na mabweni ya wanafunzi wa kike.





0 Comments