Header Ads Widget

WAZIRI MAKAMBA - MRADI WA USAFIRISHAJI BOMBA LA MAFUTA UPO HATUA NZURI, TPSF NA PSFU WAKUTANA DAR

 





Waziri wa Nishati January Makamba amesema mradi wa usafirishaji bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda kwenda Chongoleani Tanga utekelezaji wake umefikia hatua nzuri....Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Uganda (PSFU).


Amesema kuwa, lengo la kongamano hilo ni kujadili kwa pamoja mahala ulipo mradi, fursa zilizopo, masula ya mikataba, sheria, mazingira, kodi na kwa namna gani wananchi wanaweza kuzifikia fursa zilizopo.


"Asilimia 80 ya mradi huu wa usafirishaji bomba la mafuta upo Tanzania hii ni hatua moja, kuwajengea uwezo vijana katika kuzitambua na kuzifikia fursa zinazopatikana katika mradi huu kwa manufaa ya watanzania wote ni hatua nyengine"amesema Waziri Makamba.


Amesema kuwa, wao kama Serikali wanaamini kongamano hilo ni muhimu kwa Sekta Binafsi zote kwani mradi huo una uwezo mkubwa wa kuchangia uchumi katika kukuza ajira kwa watanzania na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwani mradi huo unakwenda kuzibadilisha nchi zote mbili.


"Kazi zote zimekamilika ikiwemo mikataba, kandarasi za awali za kazi za ujenzi ndogo ndogo zimeanza, bomba hili lenye urefu wa kilomita 1445 kila linapopita linatoa fursa kwa wananchi,ni muhimu kuzifikia fursa zilizopo" amesema Waziri Makamba. 



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Francis Nanai amesema kuwa, kongamano hilo linakwenda kutoa elimu kwa watanzania kuhusu mradi huo na kuyajibu maswali yote waliokua wanajiuliza kuhusu mradi huo ikiwemo masuala ya kodi. 


"Maswali yote leo kuhusu mradi huu yatapata majibu kwani viongozi wa pande zote mbili wapo, kama kuna changamoto yoyote itapatiwa majibu, watanzania kama hawaufahamu mradi huu leo watapata elimu ya kutosha ili waweze kuzifikia fursa."amesema Nanai.


Aidha, amewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika mradi huo ili waweze kunufaika kutokana na asilimia kubwa ya mradi huo kuwepo Tanzania, hivyo amewataka washiriki wasiwe watazamaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI