JESHI la Polisi mkoani Kagera limekamata watuhumiwa 124 kwa makosa ya kukutwa na nyara za serikali, mauwaji, mali ya wizi na makosa ya barabarani.
Juma amesema, mnamo Novemba 6, mwaka huu majira ya 5:00 Asubuhi katika kijiji cha Minziro Wilayani Missenyi, Polisi walifanikiwa kukamata mtuhumiwa Tawabu Ismail (35)na Joseph Laurian(42).
Amesema, watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na mfupa wa mguu wa tembo na meno matano.
Amesema, Octoba 31, mwaka huu majira ya 2:45 usiku askari walikamata raia wawili wa nchi ya Burundi Robert Berebado(19) pamoja na Benadetha Marco (19) walihusika na mauwaji ya Thropista Laurian (71).
Amesema Octoba 28, mwaka huu huko katika kijiji cha Lukimelo Kata ya Izimbya wilayani Bukoba, askari wakiwa doria walikamata watuhumiwa watano wa makosa ya wizi wa pikipiki.
Amesema Novemba 8 hadi 10, mwaka huu katika maeneo mbalimbali zimekamatwa pikipiki 146 na madereva 111kwa makosa ya kutokuwa na kofia ngumu, kuzidisha abiria na kutokuwa na leseni.CHANZO NIPASHE
0 Comments