Header Ads Widget

MAITI YAKUTWA CHINI YA DARAJA MANISPAA YA SHINYANGA.

 


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga


Mtu mmoja mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na 40 asiyefahamika jina wala makazi yake, amekutwa amefariki Dunia chini ya daraja la Ndala katika Manispaa ya Shinyanga 



Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema alituma askari kwenda kwenye eneo la tukio ambao walikuta mwili wa marehemu ukiwa chini ya daraja lakini haukuwa na jeraha lolote.



Amesema kwa sasa mwili wa marehemu uko katika Hosptali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu  ili kubaini chanzo cha mtu huyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI