Header Ads Widget

WATENDAJI OFISI YA NISHATI WATAKIWA KUSIMAMIA MAZINGIRA

 


KATIBU Mkuu Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Dk. Mngereza Miraji Mzee, amewataka wadau na watendaji katika Ofisi za Nishati, Mazingira pamoja na Ofisi za Wilaya kusimamia ili yasiharibiwe na uchimbaji wa Mchanga,Mawe na Vifusi.MWANDISHI THABITI MADAI ANARIPOTI KUTOKA  ZANZIBAR 


Akifungua kikao cha wadau cha kujadili namna ya kurejesha maeneo yalioathiriwa na uchimbaji wa Mchanga, Mawe na Vifusi ambapo kikao hicho kimefanyika katika ukumbiwa ZURA Maisara Mjini Unguja, alisema rasilimani hizo zinastahiki kurujeshwa kwa kupanda miti ili zisipotee.


Alisema baada ya muda kupita maeneo hayo yaliochimbwa rasilimali hizo zinaweza kurudi kama watafuata masharti yaliowekwa.

Alisema, serikali imeandaa taratibu za wananchi wanaotaka mchanga kwa lengo la kuendelea kuhifadhi mazingira.

Alisema lengo kuu ni suala la elimu hiyo kurejesha maeneo yaliyoathirika na uchimbaji wa rasilimali zisizorejesheka ambapo kwa huu maeneo zaidi ya saba yameathirika kuanzia mwenzi wa januari.

Alisema walifanikiwa kwa ushirikiano na wadau wengine ambao wamekuwa wakikutana na kujadili na kufikia hatua ya kurejesha maeneo hayo, hivyo serikali kupoitia idara ya nishati alikagua baadhi ya maeneo mengi yapo panga tupu.

Aidha walisema kwa sasa matatu yamerejesha ambapo lengo la serikali ni kila shimo linalochimbwa linakuwa linarejeshwa kwa kupanda miti ili tija iweze kupatikana.

Alisema serikali imekuja na mfumo wa kutaka rasilimali zisizorejesheka kwa kutumia maombi maalum ambapoo ambapo kwa sasa upo katika hatua za miwsho.

Alisema mpango huo kwa sasa kwa kiwango kikubwa ushakamilisha ambapo utakamilisha mchakato wote wa maombi ambapo mchanga kifusi utafanyika online.

Sambamba na hayo, alisema kuwa lengo la serikali ni kupunguza mianya ya kupoteza mapato ya serikali ambayo yamekuwa yakipotea sana.

Nae, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini, Muhidini Makame Haji, alisema, athari nyingi zinajitokeza kwenye kuvuna rasilimali ya mchanga kusipokuwa na kibali rasmi hivyo, ni vyema kila mmoja akaendelea kuenzi na kuitunza rasilimali hiyo ili kutotokea athari nyengine katika maeneo yaliochimbwa mchanga.

Aidha alisema lengo la kikao hicho ni kuwapatia taalum kuhusu urejeshaji wa maeneo ambayo yamechimbwa rasilimali zisizorejesheka ikiwemo mchanga.

Alisema kwa miaka mingi kumekuwepo shughuli za kuchimbwa rasilimali zisizorejesheka ikiwemo mchanga fusi na mawe ambapo imekuwa ikiacha athari kwenye ardhi.

Aidha alisema kwa taarifa zilizokuwepo hivi sasa bado hazijafanyiwa urejeshaji hivyo alisema waliona ipo haja ya kuwaita wadau ili kujadili kwa pamoja ili kuwepo uwelewa wa pamoja na namna bora ya kurejesha mmaeneoe hayo.

Hivyo, alisema kuwa matarajiyo yao ni kuleta matokeo ikiwemo kurejesha kwa kutunza mazingira na kupanda miti ili rasilimali hiyo isipotee ambapo lengo lao ni kuendeleza elimu hiyo kwa masheha na wananchi.

Akitoa mada juu ya athari zinazotokana na uchimbaji wa mchanga, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi binafsi ya kimazingira Envidec (Environmental Development for communites), Zildat Wahid Juma, alisema, uchimbaji wa mchanga unaleta athari kubwa katika mazingira ambapo kumekuwepo athari tofauti zinazokuwa zinajitokeza ikiwemo afya na kimazingira.

Hivyo, ni vyema wadau hao kuendelea kutoa elimu ili athari hizo ziweze kuwa historia ikiwemo kupanda miti ili kuridisha hali ya ardhi iliyoharika.

Alisema, janga kubwa linalotokea hivi sasa ni mabadiliko ya tabia ya nchi amabapo kunapelekea uchimbaji wa mchanga,ukataji miti ovyo,athari za kiafya ongezeko la joto na mafuriko ndiko kunapelekea kutokea  kwa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Nae Alawy Hija kutoka Mamlaka ya udhibiti wa mazingira, alisema amesema wilaya ya kati inaongoza kuchimbwa mchanga ambapo kuna hekta zaid ya 80 zimechimbwa mchanga kunapelekea athari mbali mbali za kijamii na kimazingira.

Hivyo, aliitaka jamii kuwa na mwamko wa kuendelea kuelimisha athari zinazotokea wakati wakichimba michanga ambao haupo kihalilali jambo ambalo linapelekea pia kuharibu mazingira ya sehemu.

Nao washiriki wa kikao hicho wameishauri serikali kutoa elimu zaidi hasa kwa watendaji wa chini ili kunusuru ongezeko la athari za uchiimbaji wa mchanga ambao kwa sasa umekuwa ukikithiri zaidi.

Mkutano huo wa siku moja uliwashgirikisha wadau wanaomiliki mashamba binafsi na wanaotoka katika jumuiya ya wamiliki wa mashamba, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na mabaraza ya miji Unguja pamoja na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini ambao umeandaliwa na Idara ya Mazingira na Misitu ili kuona namna bora ya kurejesha maeneo yaliyoathirika


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI