Header Ads Widget

WANANCHI WAZIBA MTO RUVU NA MAGOGO, WAZIRI AWESO AINGIA MTONI ATOA MAAGIZO MAZITO

Waziri wa maji Jumaa Aweso ameongoza jopo la wataalamu wa maji kutoka Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu,Moruwasa na Dawasa kuondoa magogo na mawe  katika mto Ruvu baada ya wananchi wa Kijiji Cha Kibangire Morogoro vijijini kuziba mto huo na kufanya shughuli za uchimbaji madini. mwandishi wa matukio daima Jacobo Sonyo anaripoti kutokea Morogoro

Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa  kuagiza kuondolewa watu wanaofanya uharibufu kwenye vyanzo vya maji ili kunusuru changamoto ya kupungua kina Cha maji katika mto huo na kusababisha mgao wa maji katika mikoa wya Pwani na Dar es lam.

Waziri Aweso alitembelea maeneo mbalimbali  ya vyanzo vya maji na kushuhudia  uharibifu mkubwa wa vyanzo hivyo ikiwemo makundi ya Mifungo katika mito inayotiririsha maji Mto Ruvu uchepushaji wa maji  na kutoa maagizo ya  kufanya  operesheni maalum ya Kuondoa wafugaji  na watu wote wanaofanya shuguli za Kibinadamu kwenye vyanzo vya mito.

"nimejionea namna watu  walivyofanya uharibifu kwa kuziba mto na kuchepusha maji pamoja makundi ya Mifugo katika maeneo ya vyanzo vya maji hivyo naagiza Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu mshirikiane na serikali za vijijini katika operesheni hii bila kuleta taharuki kwa jamii" Aweso

Mikoa ya Dar esalam ,Pwani na Morogoro imekumbwa na Changamoto ya uhaba wa maji zaidi ya mwezi mmoja Sasa kutokana na kina  Cha maji katika mto Ruvu kupungua kwa kiasi kikubwa ambapo ndio chanzo kikubwa Cha uzalishaji maji  katika mikoa hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS