MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe ,imewahukumu washtakiwa wawili Manase Mhada (25) na Mwapulise Mfikwa (@() kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Eva Merikion Mgaya (28) nyumbani kwake kijiji cha Ihanga wilaya ya Njombe.
Washtakiwa hao walitekeleza mauwaji hayo baada ya kumvamia nyumbani kwake Eva na baada ya kufika kwa lengo la kuiba mali.
Akisoma hukumu hiyo jaji Filmin Matogolo alisema tukio la mauwaji lilitokea may 8 mwaka 2015 baada ya wawili hao kwenda nyumbani kwa Wilfred Vitus Ng'olo ambaye ni mume wa mareheme wakiwa na bunduki iliyotengenezwa kienyeji ambapo walivamia na kuiba kwa kunyang'anya fedha kwa kutumia silaha .
washtakiwa hao pia walichukua simu ya mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Merikion Mgaya kifuani kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papo hapo kisha kutoweka kabla ya kukamatwa na baada ya upelelezi wa tukio hilo





0 Comments