Header Ads Widget

TMDA YAWAPIGA MSASA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA TEMEKE, JUU YA USALAMA WA DAWA

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA], imeendesha mafunzo  kwa watendaji na watumishi wa Halmashauri ya Temeke na ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuimalisha mahusiano kwenye ukaguzi waliokamisiwa ikiwemo wa madawa na vifaa tiba ikiwemo suala la udhibiti wa tumbaku.


Akizungumza katika mkutano huo, Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki, Bw. Adonis Bitegeko, alisema mafunzo hayo ya muda mfupi kwa watendaji hao, yatasaidia katika kuendelea kudhibiti bidhaa za dawa na vifaa tiba ndani ya Halmashauri hiyo.


Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko akifafanua jambo katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke .

Aliongeza kuwa, kwa mujibu kifungu namba 121 cha sheria ya dawa, vifaa tiba imebainisha majukumu ya halmashauri wanayotakiwa kutekeleza ambayo ni ukaguzi wa maeneo yanayotoa huduma ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kufatilia ubora na usalama wa bidhaa.


“Halmashauri zina uwajibu wa kufatilia ubora na usalama, kama kuna tatizo wanatakiwa kuziondoa bidhaa sokoni pamoja na kutoa taarifa TMDA” amesema Bw. Bitegeko.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Mafuku Kabeya alibainisha kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwani yanaimalisha ushirikiano katika utendaji wa ukaguzi wa dawa na vifaa tiba ndani ya hiyo ya Temeke.


“Ni jambo la muhimu kupata mafunzo kutoka TMDA na sisi tupo tayari kuyapokea kwa ajili ya wananchi wetu ili tuingie katika utekelezaji” amesema Bw. Kabeya.


Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dkt. Gwamaka Mwabulambo, amesema kuwa wataendelea kusimamia na kuthibiti ubora wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika wilaya ya Temeke.


“TMDA wapo hapa kutupa ujuzi zaidi wa jinsi gani tunaweza kutekeleza majukumu kwa kuongeza ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanapata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyo safi na salama kwa matumuzi ya binadamu” amesema Dkt. Mwabulombo.


Dkt. Mwabulombo amebainisha kuwa kila baada ya robo mwaka Manispaa ya Temeke wanafanya ukaguzi na wakibaini kuna tatizo hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa kwa hatau.


Nae Mfamasia Msaidizi Manispaa ya Temeke Bw. Bernard Sabuni, amesema kuwa changamoto iliyopo katika utekelezaji wa majukumu ya ukaguzi wamekuwa wakikutana baadhi ya watoa huduma kuwa na vyeti feki.


“Sasa hivi watu baada ya kuona kuuza dawa ni biashara, basi wengi wamekuwa wakitumia ujanja wa kugushi cheti feki, hivyo kuna utaratibu mtu akiomba kibali cha kufungua duka la dawa lazima awe na cheti orginal” amesema Bw. Sabuni.






Mfamasia Msaidizi Manispaa ya Temeke Bw. Bernard Sabuni akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI