Wanafunzi wanaohitimu katika vyuo mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuendelea kushirikiana na waalimu wao pamoja na kuwaomba ushauri wa Nini Cha Kufanya ili waweze kufanikiwa na kufikia malengo waliyojiwekea......Na Rehema Abraham
Akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya 76ya chuo Cha ufundi Moshi community center Apaikunda Naburi ,diwani wa kata ya mawenzi mkoani Kilimanjaro amesema kuwa amefurahishwa kuhitimu kwa vijana wa chuo hicho kwani wanapoondoka chuoni hapo wanakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe kwa ujuzi walioupata.
Aidha amesema kuwa ni vyema wanafunzi hao wakaenda kuyafanyia kazi kwa bidii Yale ambayo wamefundishwa kwa kutafuta shughuli za kufanya kulingana na yale waliyosoma chuoni.
"kwa Sasa hivi Kuna mikopo ya vijana ,Kuna mikopo kwa ajili ya akina mama ,mikopo ya watu wenye ulemavi, kwa hiyo Mimi nasisitiza sana hawa vijana wawe na hofu ya kwamba wanaporudi mitani ,wajiunge katika vikundi vya watu watano kwani watakuwa na Ile sifa ya kukopeshwa,wanaweza kukopeshwa wakatengeneza kiwanda chao, kikubwa wanatakiwa wawe waaminifu na wenye kujituma .
katika hatua nyingine amesema kuwa Kama vijana hao wataungana katika vikundi , yeye Kama Kiongozi atashirikiana na maendeleo ya jamii ili vijana hao waweze kupata mikopo itakayowasaidia kijiendeleza .
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo hicho Cha Moshi community center padre Dominic Kimboi amesema kuwa chuo hicho kimeanzishwa mwaka 1964 ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi ni wasichana.
"Masomo Kama usecretari wanaopenda wengi ni wasichana japo Kuna wavulana wanaojitokeza mara chache lakini sio wengi ,ila kwa fani nyingine Kama computer , hata ushonaji tulishakuwa na wanafunzi wanaume lakini sio wengi mmoja au wawili"
Hata hivyo amesema kuwa tatizo la Ajira Bado lipo kwani wanafunzi wengi wanaohitimu katika vyuo mbalimbali wamekuwa wakitafuta ajira hivyo amewashauri wanafunzi hao waweze kujiajiri wenyewe na sio kisubiri kuajiriwa.
Nao wanafunzi waliohitimu akiwemo Esta Shirima amesema kuwa kutokana na elimu aliyoipata ataweza kujiajiri na kuonesha ujuzi Alioupata kwa vitendo.





0 Comments