Katibu Mkuu Wizara ya viwanda na biashara Dk Dotto James amewasihi wahitimu wa chuo cha CBE kutokata tamaa ili kuweza kuyafikia malengo waliyojipangaia na kufanikiwa kimaisha. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza
Wito huo ulitolewa katika mahafali ya 14 ya chuo hicho cha elimu ya biashara katika kampasi ya Mwanza na kueleza kuwa kufanikiwa ni lazima kuvaa uzalendo wenye heshima ili kupata taifa lenye maendeleo.
Dk James ameeleza kuwa ni vema wahitimu hao kuwa na maadili mema ili kuweza kufikia malengo yao sanjari na kuwa wabunifu kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali kwa sababu ya uhaba wa ajira ulipo nchini.
Ameeleza kuwa kuna taasisi nyingi za kifedha ambazo zinakopesha pesa ni vema kuzitafuta ili kuweza kupata mikopo hiyo ili kufikia malengo ya kujikomboa na kuepuka kuwa tegemezi kwa familia na nchi kwa ujumla
Aidha Dk james ameeleza kuwa chuo hicho kina uwezo wa kudahili wanafunzi 2000 kutoka wanafunzi 400 hivyo Serikali itaendelea kukitizama zaidi ili kuweza kumaliza changamoto ambazo wamezibainisha.
"Lengo la serikali ni kuona chuo hiko kiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi ili waweze kupata elimu kama sera inavyotaka",amesema Dk James.
Naye Mkuu wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Emmanuel Mjema amesema kuwa wanatarajia kuwaongezea uwezo wahitimu hao kwa kuwapa mipango ambayo itawasaidia wanafunzi kuanzisha biashara zao zitakazosaidia kujiajiri wenyewe.
"Tumeanzisha mpango mwingine wa mwanafunzi asome huku anafanya kazi tumeona wanafunzi wengi hawana ujuzi wa kufanya biashara kwani kupitia mikakati hii tutawasaidia ili waweze kujiajiri na kuajiri watu wengine kwani kufanya hivyo kutapelekea kunufaika na elimu wanayoipata kutoka chuoni hapo.
Prof.Mjema aliongeza kuwa, chuo hicho kinatoa wanafunzi wenye weledi na watakaosaidia mambo mbalimbali katika jamii.
" Tunaishukru Serikali kwa kutununulia eneo hili na majengo na sisi tutaendelea kufanya vizuri kwani viongozi mbalimbali wamesoma hapa ambao hivi sasa ni Mawaziri, wafanya biashara wakubwa, hakuna kitakachoturudisha nyuma na kushindwa kuwasaidia na kuwapa ujuzi vijana hawa ili waweze kutimiza ndoto zao za baadae,"alisema prof Mjema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa chuo cha elimu ya Biashara Prof Wineasta Anderson alisema lengo kubwa la chuo ni kutoa wahitimu wanaojitambua katika tasinia mbalimbali ikiwemo ujasiliamali ili kutengeneza Taifa la watu wanaojitengemea ili wakimaliza masomo yao waweze kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Alisema wahitimu hao watakuwa mabalozi wazuri kwa kujiari na siyo kuwa tegemezi.
"Chuo hiki kinakabiliwa na changamoto mbalimbali tunaiomba Serikali iweze kututatulia zikiwemo za miundombinu ya barabara,umeme,na bweni la wanafunzi linahitaji kufanyiwa ukarabati,"alisema wineasta.
Jumla ya wahitimu 484 wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada wanaume 257 sawa na asilimia 53 na wanawake 227 sawa na asilimia 47 .
0 Comments