Header Ads Widget

WAFA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI ..

Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo watoto wawili na mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi majengo wilaya ya sikonge mkoani Tabora baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba molamu. mwandishi wa matukio daima Lucas Raphael anaripoti kutokea Tabora

Kamanda wa polisi mkoani Tabora akizungumza na waandishi wa habari jana Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea Novemba 16 mwaka huu majira ya saa 12 na 30 jioni katika shimo lililokuwa limechibwa na wachina wanaojenga barabara iliyopo katika kitongoji cha Usenga kijiji cha misheni kata ya misheni wilaya ya sikonge mkoani hapa


Alisema kwamba chanzo ni kuporomoka kwa kifusi /udogo na kuwaangukia marehemu wakati wakiwa chini wakichimba molamu hiyo.

Kamanda huyo wa polisi aliwataja walifariki kuwa ni mwanafunzi Rashid Hamis (9) Sadiki Ramadhani (9) na Bakari Shabani (21).

Aidha aliwataka wananchi wote wa mkoa wa Tabora kuchua tahadhari katika maeneo ya ujenzi ambayo kuna mashimo makubwa ili kuepukana na madhara hasa tunavyoelekea katika kipindi cha masika.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI