SERIKALI ya mkoa wa Iringa imepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na serikali chini ya rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia mkoa huo fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8.6 wa ajili ya uteelezaji wa miradi ya mapambano dhidi ya UVIO -19.Mwandishi wa MDTV Zacharia Nyamoga na Francis Godwin wanaripoti
Katibu tawala mkoa wa Iringa Happiness Seneda amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo mkoa wa Iringa wakati wa kikao maalum cha madiwani wa halmashauri zote za mkoa wa Iringa kilichofanyika Ukumbi wa Royal Pulm mjini Iringa .
Alisema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 mkoa wa Iringa umepangiwa bajeti ya shilingi Bilioni 8,680,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza Mradi namba 5441 Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Aliongeza kwa kusema kuwa hadi kufikia mwezi novemba, 2021 jumla ya shilingi Bilioni saba milioni mia nane sitini na nane mia sita sitini na sita elfu mia tatu ishirini (7,868,666,320.00) zimekwisha pokelewa katikaHalmashauri.
Pia ametolea mchanuo wa pesa hiyo ambapo amesema shilingi bilioni sita milioni mia saba (6,700,000,000.00) ni kwa ajili uya sekta ya elimu, shilingi bilioni moja milioni mia moja ishirilini (1,120,000,000.00) ni kwa ajili ya sekta ya Afya na shilingi milioni arobaini na nane laki sita sitini na sita elfu mia tatu na ishirini (48,666,320.00) ni kwa ajili ya ufuatiliaji na tathimini ya miradi inayotekelezwa nchini ya mpango huu.
Sanjari na hayo alizungumzia Changamoto za vifo vya kina Mama na kusema vifo vya kina mama vimezidi kuongezeka siku hadi siku Mkoani Iringa “Mlikuwa mnalalamika kuhusu kupigwa faini kwa wakina mama wanao jifungulia majumbani faini ile tumeitoa lakini tatizo linazidi kuongeka wakina mama hawafiki hospital wanajifungulia tu majumbani” Amesema Seneda
Kwa kumalizia amewataka madiwani kuwasisitiza wananchi katika kata zao juu ya suala zima la Afya ilikujikinga na magonjwa mbalimbali yanayo samba na amewataka wanachini kuwa na tabia ya kujua Afya zao kwa kwenda hospital kujua Afya zao na kupata matibabu.
Hata hivyo MNEC Salim Asas ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ulio wakutanisha madiwani mkoa wa Iringa alipokuwa akizungumza amewaasa wakazi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kujikinga dhidi ya UVICO-19 kwa kufuata ushauri tunaopewa na wataalamu wa Afya ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa.
Mkutano umefungwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dr Nyamhanga huku akiwataka Madiwani kuyafanyia kazi yale waliyo afikiana kwa kuyaweka katika utekelezaji ili kuyafikia maendeleo amesema kama wasipo yafanyia kazi yale waliyo afikiana haita saidia kitu.
Kwa kumalizi haya pia alisema wapo katika utaratibu kuhakikisha kuwa wana wainua wakina mama katika kuwapatia mikopo yenye tija na riba nafuu “Ifike mahala tuache kuwapa mikopo kama vipande vya nyama unakuta watu wapo 10 unawapa shilingi milioni moja yaani wagawane shilingi laki moja moja si kwelii jamani pesa hiyo itaishia katika kununua madela na vyombo tu na sikumuinua mwanamke” alisema Dr Nyamhanga
0 Comments