Header Ads Widget

MKUU WA POLISI WILAYA NAMTUMBO AWATAKA WANAFUNZI NA RAIA WENGINE KUZINGATIA ELIMU YA USALAMA BARABARANI.

 




MKUU wa Polisi wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma William Mwamafupa  amewataka Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari  pamoja na Raia wa kawaida wa  Wilayani humo  kuzingatia elimu ya usalama barabarani pindi wanapozitumia barabara hizo ili kuzuia ajali ambazo asilimia kubwa hutokana na uzembe wa utumiaji wa barabara ikiwemo na watuaji wa vyombo vya moto....NA AMON MTEGA, NAMTUMBO.



 Mwamafupa ambaye alikuwa mgeni rasmi ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ,ambayo yamefadhiliwa na kampuni ya Mantra Tanzania Limited inayojishughulisha na madini ya Urani yaliopo katika mto Mkuju Wilaya ya Namtumbo mkoani humo .




  Mkuu huyo amesema kuwa kama jamii wakiwemo wanafunzi ikazingatia suala la usalama barabarani basi itasaidia kupunguza(Kuzuia) vitendo vya ajali barabarani ambazo zimekuwa zikigarimu maisha ya watu na kuzifanya baadhi ya familia kuwa masikini.




  Hata hivyo mkuu huyo ameipongeza na kuishukuru kampuni ya mantra kwa kutoa ufadhili wa mafunzo hayo ambapo hadi kuhitimisha shule 23 za Msingi na Sekondari zimepatiwa mafunzo ya usalama barabarani huku fedha Sh.Milioni 9.4 zilitolewa na kampuni hiyo kwaajili ya kuendeshea mafunzo hayo.





  Naye mkuu wa kitengo cha usalama barabarani katika Wilaya ya Namtumbo Evans Myombe amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakipata ajali kwa uzembe wa kutokuchukua tahadhari ya kutokutambua sehemu sahihi ya waenda kwa miguu pamoja na wa vyombo vya moto.




 Pia Askari Polisi anayesimamia dawati la Jinsia katika Wilaya hiyo Mwanaisha Monyo amesema kuwa licha ya suala la usalama barabarani lakini bado usalama hatarishi hasa kwa wanafunzi wa kike ambao baadhi yao hubakwa huku wazazi wao kutokutoa taarifa kwenye vyombo husika jambo ambalo lifanya vitendo hivyo vya kikatili viendelee kuwepo.






 Mwanaisha amewaambia baadhi ya wazazi waliokuwa kwenye ufungaji wa mafunzo hayo kuwa wakapeleke ujumbe na kwa wenzao ambao hawakuwepo kwenye mafunzo hayo kuwa wawe na mazoea ya kuwakagua watoto wao hasa wakike ili kutambua kama wanafanya vitendo viovu.



Meneja uhusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania Limited Khadija Pallangyo


 Kwa upande wake Meneja uhusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania Limited Khadija Pallangyo amesema kuwa kampuni hiyo imefadhili mafunzo hayo baada ya kutambua baadhi ya Wananchi wakiwemo Wanafunzi wamekuwa hawafahamu suala zima la usalama barabarani.




 Meneja uhusiano huyo amesema kuwa licha ya kufadhili mafunzo hayo lakini bado kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na jamii katika utekelezaji wa miradi mbalimbali

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI