Maduka ya Soko la Manzese lililopo kata ya Tunduma ndani ya Mji wa Tunduma yameungua na kuteketea kwa Moto saa 11 alfajiri ya Leo tarehe 16/11/2021
Akiongea na wananchi katika eneo la Ajali ya moto huo Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Fakii Lulandala amesema Maduka 43 yameungua kati ya Maduka 746 ya Soko la Manzese na mpaka sasa bado thamani Halisi ya Mali zilizoungua haijajulikana.
Kati ya Vyumba 43 vilivyoungua 33 vilikuwa ni Maduka yenye bidhaa na 10 vyumba tupu ambavyo vilikuwa havijaanza kufanyiwa biashara
Mhe. Fakii alitoa maagizo kwa kuunda Tume ya uchunguzi wa chanzo cha Moto huo ambao umeteketeza Maduka na Mali nyingi za wananchi
Pia aliwashukuru wananchi kwa kusaidiana na Jeshi la Zimamoto katika kuokoa moto huo usiendelee kushika katika Maduka mengine zaidi.
Mhe. Fakii alilishukuru Jeshi la Polisi la Tunduma kwa kuhakikisha ulinzi na usalama wakati wa ajali hiyo ya moto. Kwani baadhi ya wananchi ambao sio waaminifu hutumia mwanya huo na kubomoa maduka jirani na kuiba mali za wananchi.
Wananchi waliounguliwa Maduka yako wameiomba Serikali kuwasaidia Kwani Mitaji yao imeungua na wanamikopo Benki hivyo wanaomba aliyehusika kwa uzembe na kusababisha moto awajibishwe hata kama iwe ni taasisi ya Serikali. Kwani wao hayo Ndio maisha yao na wanategemea kulipa Mikopo, kusomesha watoto, na mahitaji yote ya familia.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Fakii Lulandala amewaomba wahanga wote wawe na utulivu Katika kipindi hiki ambacho uchunguzi unafanyika na taarifa ataitoa pindi Kamati hiyo itakapomaliza uchunguzi.
Chanzo cha Habari :Tundumatc
0 Comments