Header Ads Widget

KIJANA WA MIAKA 31 AKAMATWA KWA KUBAKA NGURUWE ALIYEKUWA AMEFUNGWA KAMBA KWA AJILI YA KUCHINJWA

Picha  hizi  ni  za mtandaoni  hazihusiani na tukio la kijana wa  Ludewa 

WAWEZA kusema ni  dalili za mwisho wa  dunia  kutokana na matukio ya kushangaza kuendelea kujitokeza , kijana  Afro Nyigu (31) mkazi wa kijiji  cha Mavanga  kata ya Mavanga wilaya ya  Ludewa mkoa  Njombe  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumbaka mnyama aina ya Nguruwe.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Ramadhani Kihanga amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 14 2021 ambapo mtuhumiwa huyo alifika katika machinjio ya wanyama hao huku akiwa amelewa na kukuta nguruwe akiwa amefungwa kamba kwa maandalizi ya kuchinjwa ndipo kijana huyo alimvamia na kufanya nae mapenzi.

Alisema wakati akiendelea na tendo hilo mlinzi wa machinjio hiyo alikuwa ametoka kidogo na aliporejea alimkuta kijana huyo akiendelea kufanya kitendo hicho ambapo alimkamata na kumpigia simu balozi na mtendaji wa kijiji ambao walifika katika eneo hilo la tukio.

Alisema kuwa walipomuhoji kijana huyo sababu za kufanya kitendo hicho alidai ni maamuzi yake binafsi hivyo hapaswi kuulizwa ambapo viongozi hao wakamchukua na kumkabidhi mikononi mwa polisi.

“Kitendo alichokifanya huyu kijana mwenzetu ni cha kusikitisha sana! Tunaomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine maana kama ameweza kufanya hivi kwa mnyama anaweza kufanya uharibifu hata kwa binadamu”,

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Njombe Hamiss Issa amethibitisha  kutokea kwa  tukio hilo na kuwa  wanaendelea na uchunguzi  zaidi .

Matukio  daima Media   tunaungana na  wote wanaoendelea  kuliombea Taifa amani  na  kuepukana na matukio ya ajabu kama haya 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS