Header Ads Widget

TAKUKURU MBEYA KUFUATILIA FEDHA ZA UVICO 19

Na  Matukio daima media,Mbeya

MKUU wa Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya,Denis Manumbu ametoa onyo kali kwa watendaji na viongozi  watakaobainika katika ufujaji wa fedha za Ugonjwa wa Uviko 19 ambazo zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo  katika sekta ya Afya, Elimu na barabara.

Manumbu amesema hayo jana wakati akizungumza na Wanahabari ofisini kwake juu ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya mwaka kuanzia julai hadi septemba.

Aidha Manumbu aliema kuwa  tayari Serikali imeingiza fedha za Uviko 19 kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya na kuwaomba watendaji na viongozi wote wa serikali  wote watakaopewa nafasi ya kusimamia miradi kuwa waaminifu kujiepusha na vitendo vya rushwa.

“Nawatahadharisha watumishi wote wa umma fedha za Uviko 19 zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa  kila Halmashauri imepewa fedha, tunaendelea kufuatilia na kufanya uchunguzi kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Manumbu.

Hata hivyo Manumbu alisema kwamba kazi ya kuzuia na kupambana na rushwa itaendelea katika maeneo yote zikiwemo taasisi za umma na binafsi na kushauri namna bora ya kuiziba mianya hiyo.

"Natoa rai kwa wakurugenzi wa halmashauri zote za.mkoa wa mbeya kutoa ushirikiano wa hali ya juu wakati wa kutekeleza miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uvico 19 katika tawala za.mikoa na mamlaka za serikali za mitaa pindi utakapo hitajika"alisema Kamanda wa Takukuru.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI