Header Ads Widget

WANAHABARI WATAKIWA KUTANGAZA UTALII

 


Editha Karlo,Mbeya


MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Rashid Chuachua amewataka wanahabari kutangaza vivuvitio vya utalii pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo katika Wilaya hiyo.


Dk Chuachua amewaalika wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali Tanzania kwenda Mbeya kuwekeza  Ili kunufaika na   fursa mbalimbali za kiuchumi.


Hayo aliyasema wakati akizungumza na Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao walifanya ziara mkoani Mbeya  kwa lengo kutangaza vivutio vya utalii na fursa uwekezaji zilizopo katika Mkoa huo.


Alisema Mkoa wa Mbeya umebarikiwa kuwa na maeneo mazuri ya uwekezaji yenye kuvutia pamoja na miundombinu rafiki ambayo  inafaa kuendesha shughuli za uzalishaji.


HataHivyo  Dk. Chuachua aliwaomba wanahabari hao kusaidia kuutangaza Mkoa wa Mbeya pamoja na fursa zilizopo ili kukuza uchumi wa Mkoa na mtu mmoja mmoja kupitia uwekezaji unaofanywa na kuzalisha ajira.


Baadhi ya Wanahabari waliopo katika ziara hiyo Salma Mrisho mwandishi wa star Tv Mkoa wa kutoka Mkoa wa Geita k alisema Mkoa wa Mbeya umebarikiwa kuwa na ardhi nzuri ambayo inafaa  uwekezaji wa kilimo,na mazao yatakayopatikama yanachakatwa na kuuzwa maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi na hata nje ya nchi.



Aliongeza kuwa uwepo wa madini katika Wilaya ya Chunya kumechangia idadi kubwa ya watu kujiajiri na kuajiriwa sambamba na kuongeza pato na Halmashauri.


Naye  Mkurugenzi wa Shule za Paradise Pre and Primary School, Ndele Mwaselela aliwahidi wanahabari hao kuwaunga mkono katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na uwekezaji nchini ili kufungua fursa za ajira na kukuza uchumi wa mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.


"Mmeanzisha kitu kizuri hili wazo lenu linalenga kumuunga mkono Rais wetu mama Samia Suluhu kutangaza vivutio vyetu vya utalii, nimependa nipo tayari kuwaunga mkono na nipo tayari kuwa baba mlezi wenu,mkitoka hapa kaandaeni mpango kazi wenu mniletee"alisema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI