Na Mwandishi wetu, Tandahimba
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imehasisha wakulima wa zao korosho kujiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa ili kuweza kupata matibabu katika hosptiali za serikali ziliozopo ndani ya wilaya yetu na nje.
Akizungumza na wakulima wa kijiji cha Namikupa wakati wa mnada wa sita wa korosho uliofanyikia kijijini hapo mratibu wa mfuko wa afya ya jamii (ICHF) iliyoboreshwa Wilaya ya Tandahimba Violeth Mahembe alisema kuwa wakulima wanapaswa kujitoa wakati huu ambao wanafanya mauzo ya korosho na kujiunga katika mfuko huo kwa faidia ya baadae.
Alisema kuwa kupitia mfuko huo mwanachama anaweza kupata huduma za afya katika hospitali ya wilaya na vituo mbalimbali vya serikali ndani ya wilaya ya tandahimba.
“Kwa muda huu ambao tunapesa tuwekeze kwenye afya ili kujikinga kiafya ukiumwa huwezi kuokota koroso wala kuja kwenye mnada”
“Tunaomaafisa waandikishaji hao wapo kwenye kila kijiji wanatusaidia kutekeleza majukumu yetu kwa ngazi hiyo”
“Mfuko wa afya ya jamii unatoa huduma za afya kwa watu wote nchini unatakiwa ujiunge kwa gharama ya shilingi 30 kwa watu sita wote mnapewa kadi maana ya watoto mama na baba ndani ya hosptili za wilaya na mkoa nasasa wameboresha hata uwe nje ya mkoa wa mtwara unapata matibabu bure”
“Wanafunzi wakiwa sita wanachanga 5000 kisha wanajiunga na kupata usajili na kunufaika kwa mwaka mzima na pia huduma hizi zinagharamia huduma zote ikiwemo e-ray, kulazwa ama utra sound kwa hospitali ya wilaya hadi ligula kokote”alisema Mahembe
0 Comments