Header Ads Widget

SALAAM KWA ANTONY MAVUNDE

 



Adeladius Makwega

Dodoma


Novemba 11, 2021 nitaka niandike jambo lingine lakini nilipofika kituo kimoja cha bodaboda, nilipanda boda moja kunipeleka huko niendapo, nikiwa njiani kijana huyu wa bodaboda aliniambia analo jipya moja juu ya yeye kupatwa na msiba wa shangazi yake aliyekuwa akiumwa kwa muda mrefu. 


Kijana huyu aliniambia kuwa shangazi yake alikuwa kidogo ana mali za kutosa haswa ngo’mbe lakini hakuwa na mume wala hakujaliwa kupata mtoto.Kijana huyu ansem kuwa shangazi yake alikuwa na maeneo ya kutosha ujio wa makao makuu maeneo yake mengi aliuza na kununua ng’ombe wa kutosha.


Aliniuliza kuwa je mali hizo ni za nani kwa sasa? Kwa mawazo yangu nilimwambia kuwa kama mama huyu hajaandika wosia wowote wa kumuachia mtu yoyote mali hizo basi mali zote alizokuwa anamiliki kwa makabila yanayochukua ukoo kwa baba kama Wagogo mali hizo zitakuwa mali wa ndugu wa kiume wa marehemu.


Kijana huyu alinijibu kuwa tangu shangazi yake alipokuwa mgonjwa, baba yake (kijana wa bodaboda) alikuwa akiwapangia zamu ya kuzipeleka machungani ng’ombe hizo zilizo nje ya jiji la Dodoma na jambo hilo lilikuwa kama usumbufu kwao kwnai wakiwa zamu za kuchunga shughuli zao za bodaboda zilikuwa zinakwama. Kijana huyu anasema kuwa shangazi yake (marehemu) alikuwa na kaka mmoja tu ambaye ni baba wa kijana huyu.

 

Nikamwambia kwa hakika mtu wa kwanza wa kusimamia mali hizo ni baba yake lakini hilo mnaweza kuliweka sawa pale wanandungu mtakapokaa kikao hicho ili kukamilisha  taratibu za mirathi.

 

Pengine shangazi yenu alitoa wosia wa mali hizo au pengine alikuwa na mume, nilimwmabia kijana huyu. Aliniambia kuwa wameshamzika shangazi yao tayari sasa wanangoja kikao cha wanandugu tu.


Kijana huyu aliniambia kuwa alipofariki shangazi yake walienda kuchukua miwili hospitalini na alitegemea kuwa hapo awali kulikuwa na utaratibu wa kutumia gari la Jimbo la Dodoma ambapo mbunge wa jimbo hilo Antony Mavunde alinunua magari mawili ya kubebea wagonjwa na wafu.


Lakini kijana huyu anasema kuwa magari haya kwa sasa yameharibika na zoezi hilo lililokuwa msaada wa kubeba miili ya wafu sasa yako juu ya mawe hivyo wananchi wamekuwa wakisafirisha miili yao kwa kutumia mbinu za awali kwa kuchangishana.


Kijana huyu alinisimulia kuwa utaratibu huu wa magari haya ya mbunge ulikuwa mzuri sana kwani watu wakifiwa walikuwa wakiwasiliana na ofisi ya mheshimiwa huyu na kweli walipatiwa gari hilo la kisasa la kusafirisha miili ya watu wao kwenda kuzika ndani ya Dodoma.


KIjana huyu alikwenda mbali kabisa akasema kuwa tangu mbunge wao aondolewe Unaibu Waziri, magari ya kubeba miili ya wafu ya Mbunge Mavunde hayafanyi kazi kabisa. Nilimtania kuwa sasa kwanini msichangishane yatengenezwe? Akasema hilo linawezekana kabisa lakini hadi mheshimiwa aseme. Nikamtania pia kuwa unataka kila mbunge wa Dodoma awe waziri? Kijana huyu alijibu kuwa angefurahi sana kama mheshimiwa Mavunde ambaye ni mbunge wake angekuwa waziri. 


Kwa kuwa mheshimiwa Antony Mavunde ni mtu ninayemfahamu nilijiuliza maswali mengi sana. 


Kwanza nilikumbuka kuwa mheshimiwa Mavunde nilimfahmu kwa karibu na kwa mara ya kwanza akihudumu katika Wizara ya Vijana ya wakati huo akiwa Naibu Waziri na Waziri wake akiwa ni Dada yetu mpendwa Jensta Mhagama.


Nilimfahamu mheshimiwa huyu kupitia kwa mbunge wa Jimbo la Mlalo Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga ndugu yangu Rashidi Shangazi. Kuna wakati ilinibidi kuwasiliana na mheshimiwa huyu moja kwa moja kwa simu ili kukamilisha miradi fulani wa vijana. Mara ya pili mheshimiwa huyu nilipata wasaa wakukutana naye uso kwa uso alipofika huko Wilayani Mbozi Mkoani Songwe ambapo alifika kuzungumza na vijana wa wilaya hiyo namna ya kunufaika na mfuko wa vijana.


Mara baada ya kikao hicho mheshimiwa alinipa namba yake ya simu na mimi kuchukua yake na sote tulibaini kuwa kila mmoja anayo namba ya mwenzake. Vipi imekuwaje ? (aliuliza mheshimiwa huyu) nilimjibu kuwa tuliwahi kuwasiliana kupitia kwa mheshimiwa Rashidi Shangazi nikiwa Lushoto juu ya mradi wa nyuki wa vijana, hapo hapo mheshimiwa huyu alikumbuka.


Mheshimiwa Mavunde ni miongoni mwa vijana ninaowaheshimu sana kama alivyo ndugu yangu Rashidi Shangazi. Kwa hiyo mtu unayempenda na kumuheshimu pale anapotajwa kwa namna yoyote ile ni vizuri kumjulisha ili aweze kulifanyia kazi jambo hilo.


Haya yote niliyakumbuka nikiwa katika bodaboda hiyo ya kijana huyu ambapo nilimwabia kuwa ngoja nitamkumbusha mheshimiwa ayatengeneze magari haya ya wagonjwa si kwa kutumia pesa yake ya mfukoni tu bali hata pesa ya wadau wengine ili magari haya mawili aliyoyanunua yaweze kutusaidia kutusafirisha sote tuwe wagonjwa au tukiwa wafu.Maana siku hizi na siye tupo Dodoma na magari haya ni mkombozi  kwa kila mmoja wetu



makwadeladius@gmail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI