Header Ads Widget

RED CROSS WATAKIWA KUANDAA PROGRAMU ZA UOKOZI MASHULENI

 



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph  Mkirikiti leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Red Cross Mkoa wa Rukwa  ambapo amewataka waandae programu ya maokozi kwenye shule za Rukwa ili vijana wengi wawe na umahili wa kuokoa jamii pale majanga yanapotokea... Na Elizabeth Ntambala 


Mkirikiti amesema hayo leo ofisini kwake mjini Sumbawanga pia ameupongeza uongozi wa Red Cross kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwenye jamii ya Rukwa huku akiwataka wawe na ushirikiano na Skauti pamoja na Jeshi la Zimamoto.


"Hamasisheni kampeni ya Damu Salama kwenye mkoa wetu mkishirikiana na Hospitali zetu za Halmashauri hususan maeneo ya vijijini hatua itakayosaidia kuokoa maisha ya watu " alisema Mkirikiti 


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti  wa Red Cross Rukwa Saada Kimanta ameomba ushirikiano na uongozi wa mkoa ili watambulike na kupewa kipaumbele kwenye utekelezaji wa malengo ya Red Cross.


Aliongeza kusema Red Cross tunahitaji kushirikishwa kwenye shughuli za mkoa na kitaifa ikiwemo ziara za viongozi wa kitaifa pia shughuli za usafi na uokoaji.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI