Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amewaonya wafanya biashara waliopandisha bei za vifa vya ujenzi katika mkoa wa Kagera kuacha tabia hiyo mara moja kwani hawana nafasi katika mkoa huo.Mwandishi Titus Mwombeki-MTDTV anaripoti toka KAGERA
Ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa huo ulioudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo,mkuu wa wilaya ya Bukoba, wakurugenzi,wakuu wa ulinzi na usalama pamoja na walimu wakuu wa shule za sekondari wa mkoa huo ili kujadili maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyodhamiliwa kujenga kutokana na fedha zilizotolewa na serikali kwaajiri ya ujenzi wa vyumba hivyo.
“Kuna baadhi ya wafanya biashara wameanza kuongeza bei za bidhaa mfano wilaya ya Misenyi kuna baadhi ya wafanya biashara wameongeza bei simenti kutoka shilingi elfu 21,000 hadi elfu 23,000 kwa mfuko mmoja wa simenti, nimemuita katibu wa biashara hapa tuzungumze naye pamoja na watendaji wakuu upande wa wilaya kama wao ndo wanawashawishi hapa hawana nafasi, katibu wa wa biashara nakuagiza kaongee na wafanyabiashara wako hapa hatuna nafasi ya kuongeza bei wala hapa hatuna nafasi ya mtendaji yeyote katika mkoa huu ya kuongeza bei ya bidhaa yoyote”
Amesisitiza kuwa amepita katika sehemu mbalimbali ili kukagua ujenzi wa madarasa hayo katika wilaya Bukoba mjini na kuona kuna mapungufu mengi na kusisitiza kuwa kuanzia sasa hataki kuona tatizo hilo tena katika mkoa huo kwani fedha zishatolewa zinatakiwa kutumika ipasavyo ilikukamilisha ujenzi wa vyumba vya hivyo kwa muda alioutoa.
“Nimetembelea maeneo mbalimbali katika mkoa wetu nimeona saiti nyingi haziko hai kwamaana hakuna mawe yakutosha,mchanga,simenti pamoja,matofali na kokoto sasa basi kwasababu fedha hizo ziko ndani ya mkoa wetu na ndani tya wilaya yenu hii ya Bukoba mjini kuanzia Sasa sitahitaji kupita katika saiti yoyoye ile nikute matizo kama haya, huu sio muda wa kuchezeana chezeana nataka ifikapo tarehe 30 mwezi Novemba mwaka huu ujenzi wa vyumba hivi uwe umekamilika”
Naye mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Machali amewataka wakurugenzi kupitia idada ya fedha ya elimu kuwa wepesi na kuhakikisha wanawasaidia wakuu wa shule wanawapa huduma kwa wakati wanapotaka msaada wao ili kusaidia shughuli hiyo kukamilika kwa wakati.
“Sote tunajua kuwa walimu wakuu wanapokuwa wakitakata mahitaji mbalimbali iliwaweze kupatiwa fedha baada ya kuchakata mahitaji yao huja kwenu,awawezi kufanya kazi peke yao bali wanahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi hivyo basi wakurugenzi kwa kushirikiana na idara ya fedha ya elimu kuweni wepesi katika kuwasaidia mambo mbalimbali kama vile kuweka sahihi ili waweze kurahisisha kazi zao na kuhakikisha ujenzi wa vyumba hivyo unakamilika Kabla ya tarehe 30 mwezi huu kama alivyosema mkuu wa mkoa”
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Hamugembe na mwenyekiti wa wakuu wa shule manispaa ya Bukoba Melania Bubelwa ameishukuru serikali ya awamu ya sita ikiongozwa rais Samia Suruhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwaajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kwani kulikuwepo na upungufu wa miundombinu katika mkoa wa Kagera hali ambayo ilikuwa inasababisha mrundikano mkubwa sana wa wanafunzi madarasani.
“Ujenzi huu ukikamilika itasaidia kutupinguzia tatizo la murundikano wa wanafunzi madarasani kwani imekuwa ni tatizo kubwa sana ,katika suala la taaluma unapofundisha wanafunzi inatakiwa uwe na namba ya wanafunzi angalau 40 au 45 katika darasa moja lakini wanafunzi wamekuwa wakikaa madarasani wengi sana hali ambayo inaleta shida katika ufundishaji kwa walimu, kwahiyo ujenzi wa madarasa ukikamilika suala la taaluma litakuwa limeboreshwa walimu watafundisha kwa urahisi maana namba ya wanafunzi darasani itakuwa imepuyngua”
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa zaidi ya Bil.20 katika mkoa wa Kagera kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 881 katika mkoa mzima ili kutatua changamoto ya murundikano wa wanafunzi darasani katika mkoa huo.
0 Comments