Na Fatma Ally, MDTV Dar es Salaam
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambae pia ni diwani wa Kata ya Vingunguti Omar Kumbilamoto amewataka wananchi wa Kata hiyo kupuunza maneno yanayotolewa na vyama vya upinzani kuhusu kata hiyo kutokua na maendeleo.
Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua kwenye mkutano wa wananchi ambapo ajenda ni kuzungumzia maendeleo ya kata hiyo ambayo yamefanyika kwa mwaka moja tangu kuchaguliwa kwake kwa awamu ya pili.
Amesema kuwa, yeye kama Diwani na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana Serikali amefanya mambo makubwa katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
"Miradi mikubwa imetekelezwa vingunguti ikiwemo machinjio ya kisasa na sasa tupo katika harakati za kujenga soko la kimataifa la tayari tumeanza kulipa fidia nyumba zilizokaribu na eneo la ujenzi lengo ni kupanua soko kubwa zaidi, barabara ya barakuda inakaribia kumaliza"amesema Kumbilamoto.
Aidha, amesema kuwa, kuna baadhi ya watu wanapanga njama za kumchafua kwa maneno ya kejeli kwa madai ana roho mbaya jambo ambalo ni uongo kwani alikabidhi gari la wagonjwa zahati ya Vingunguti yenye thamani mill 36, pamoja na mashine ya kufulia wakati mke wake akifulia mikono.
Hata hivyo ameipongeza kamati za shule katika Kata ya Vingunguti kwa kufanya vizuri katika mitihani ya darasa huku akiwataka wazazi na walezi kuwa na tabia ya kufatilia maendeleo ya watoto wao a kushiriki vikao vya shule Ili kutoa michango kwa ajili ya kuleta maendeleo ya watoto.
0 Comments