Header Ads Widget

NEEMA YAWASHUKIA WANANCHI WA KAGERA.

 


Na, Titus Mwombeki-MTDTV KAGERA.

Ajira 1000  zinatarajiwa kutolewa na kampuni ya Tembo Nickel corporation kwa wakazi wa mkoa wa Kagera baada ya kampuni hiyo  kumaliza mchakato wa upatikanaji wa lesseni na kupewa  baraka  rasmi na mkuu wa mkaa wa kagera ya  kuanza kwa mradi wa uchimbaji  madini katika wilaya ya Ngara mkoani kagera.  


Hayo yamesemwa na Meneja Mkazi wa Tembo Nickel Tanzania Benedict Busunzu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ulioko  mjini Bukoba na kusema kuwa takribani ajira elfu moja (1000) zinatalajiwa kutolewa katika  kipindi tofauti tofauti kuanzia kipindi  cha ujenzi wa mradi huo.


“Fursa za ajira na huduma kwa mradi zitaendelea kubadilika kwa hawamu tofauti tofauti za mradi, unatarajiwa kuwa matika kipindi cha ujenzi  takribani ajira 1000 kupitia wakandarasi wetu zitahitajika na kipaumbele cha ajira na mafunzo itakuwa kwa wakazi wa mkoa huu” amesema Meneja Busunzu.



Ameongeza kuwa kufuatia  ruhusa rasmi iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera kwa kampuni ya Tembo Nickel tutawashirikisha viongozi waandamizi wa mkoa pamoja na wanakijiji wanaozunguka eneo la mradi huo.


“Kwakupata baraka hizi kutoka kwa mkuu wa mkoa maana yake kwasasa tunaanza rasmi kushirikiana na wanajamii wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka eneo la mradi ilikuanza shughuli zetu rasmi”.


Amesisitiza kuwa katika mradi huo serikali itanifaidika pia kwani katika mkataba uliosaini kati yao na serikali walikubaliana kuwa katika uzalishaji wa madini serikali itapata asilimia 16 na Tembo Nickel asilimia 80 na katika mapato yatakayopatikana kampuni ya Tembo Nickel itapata asilimia 50 na serikali itapata asilimia 50.


Kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ameushukuru uongozi wa Tembo Nickel Corperation kwa kuanzia mkoni hapo na kwaakikishia kuwa wajisikie wako nyumbani na serikali itakuwa bega bega nao ili kuakikisha wanafanya kazi zao vizuri.


“Ni historia kwa nchi yetu hasa mkoa wetu wa Kagera   kuwa na mradi mkubwa kama huu, uanzishwaji wa mradi huu unaendana na fursa na neema kwa wananchi wa mkoa wa kagera na taifa kwa ujumla kwani kutoa itasaidia kutoa  huduma mbalimbali za kijamii mfano, chakula,mafuta, BIMA, maligafi za ujenzi wa magodauni likiwemo la saruji, nondo pamoja mabati, kupitia fursa hii wananchi wa mkoa wa Kagera watajipatia fedha na kipato pamoja na kulipa kodi”.


Aidha amesema kuwa kupitia mradi huo serikali inategemea kupata makusanyo mengi kutoka katika halmashauri ya Ngara kwani halmashauri hiyo itaanza kupata mapato kuanzia hatua ya awali ya ujenzi wa mradi. 


Ikumbukwe kuwa mradi huu ulisainiwa na aliyekuwa rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli  na kampuni ya Tembo Nickel katika mkoa wa Kagera mnamo tarehe 19 Januari  mwaka huu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI