Na Hamida Ramadhan Dodoma
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja ametoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa za taharuki zinazoendelea kusambaa katika ya mitandao ya kijamii kwamba Serikali imaruhusu usafirishaji wa wanyama pori nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa naibu waziri huyo amesema mnamo tarehe 17 machi 2016 Serikali ilitoa tamko la kuzuia ukamataji na usafirishaji wa wanyamapori hai nje ya nchi.
Amesema kuwa , baada ya hatua hiyo, Serikali iliamua kuwarejeshea wafanyabiashara wa wanyampori hai kiasi cha shilingi 173,289,430.60 ikiwa ni nia ada mbalimbali walizolipa kabla ya kusitishwa kwa biashara hiyo.
Aidha , katika ufumbuzi wa kudumu kufatia malalamiko ya wafanyabiashara, Wizara iliunda kamati ya waataalamu kwa ajili ya kufanya tathimini ya biashara ya kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi na kuishauri Serikali kuhusu hatma ya biashara hiyo.
‘’ Baada ya tathimini ya kamati ya wataalamu , Wizara imeamua kufungua biashara hiyo kwa kuruhusu usafirishaji wa wanyamapori haikwa shaghuli za utafiti wa kisanyasi na kidplomasia tu ,’’amesema Naibu waziri huyo.
Hata hivyo, amewataja wanyamapori hai ambao wanaruhusiwa katika usafirishaji katika kipindi cha mpito ni makundi ya wadudu ( invertebrates) na wanyama pori jamii ya ndege, reptilian, mammalia na amphibian, ambao jumla ni aina 617 za wanyamapori walioko kwenye mazizi.
Sambamba na hilo, amesema kwa sasa Serikali inaanda utaratibu wa kuruhusu biashara ya usafirishaji kwa wanyama pori waliokauushwa na mazao ya wanyamapori yaliyoongezwa thamani na itafanywa na wafanya biashara wenye miradi ya ufugaji wanyamapori ili kuongeza tija na kuhamasisha ufugaji wa wanyamapori.
‘’ Utaratibu huu utakapoanza kutumika na kuwezesha wafanyabiashara wetu kuwekeza zaidi kwenye ufugaji wa wanyamapori pia utasaidia kulinda kulinda sekta ya utali kwa kuendelea kuwavutia wageni kuja nchini kuona wanyamapori hai wakiwa kwenye mazingira yao ya asili’’ amesema.
MWISHO
0 Comments