Na Hamida Ramadhan Dodoma
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuthamini na kutumia matokeo ya tafiti zinazofanywa na watafiti mbalimbali kwani tafiti hizo zimekuwa zikitatua changamoto za watanzania
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo wakati akifungua Kongamano la tatu la Utafiti kwa maendeleo Jumuishi ambapo amebainisha kuwa bila kuwekeza katika tafiti shughuli za kimaendeleo zitakwama.
"Sasa kutokana na hilo nikitake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM na Vyuo Vikuu vingine vikazane kufanya tafiti na kutoa mchango wa kitafiti katika Afrika na duniani kote ili nchi yetu iweze kuwemo katika nchi zinazotoa mchango wa kitafiti katika dunia kwani kwa hivi sasa bado hatujafikia huko," Amesema Profesa Mkumbo .
Pia ameishukuru serikali ya nchi ya Swedeni kuendelea kutoa ushirikiano na serikali ya Tanzania katika shughuli za kitafiti na kusisitiza na kuomba ushirikiano huo uendelee kudumu.
" Huu ni uweli kwamba wengi wenu waliopo hapa kwenye hili Kongamano wamaepata mafunzo ya shahada za uzamili na uzamivu kupitia serikali ya nchi ya Swedeni na Ushirikiano huu umeanza muda mrefu na tunaendelea nao vizuri kwa kushikiana kwa karibu katika shida na hata kwenye raha na kwaniaba ya serikali tunawashukuru," amesema Profesa Mkumbo
Aidha alitoa msisitizo kwa watafiti kufanya utafiti zenye tija amabo zitakwenda kutatua changamoto katika jamii na hatimaye maendeleo kupatikana kwa kila mtanzania.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema katika kongamano hilo watapata matokeo ya utafiti yaliofanyo na watafiti waliopo kwenye mradi wa ushirikiano katia utafiti wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam na SIDA.
Amesema tafiti zote zinazofanyika zinalenga kutatua changamoto ya wananchi na ndio maana katika chuo cha UDSM kina Naibu Makamu mkuu kwa upande wa utafiti lengo kuona zile tafiti zilizofanywa zinawafikia watanzania.
" Sisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM tunasema kuwa tafiti ndio kila kitu kwani tumekuwa tukifanya tafiti sio tu kujifurahisha bali ni kwaajili ya maendeleo ya wananchi wote wa mijini na vijijini," amesema Profesa Anangisye
Mwishoo
0 Comments