Header Ads Widget

MRADI WA MATUMIZI YA MITANDAO KWA WANAWAKE WAZINDULIWA ARUSHA

Mradi wa Kuwajengea uelewa na ujasiri Wanawake Vijana walioko kwenye Taasisi ya elimu ya juu kuweza kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi wanafunzi umezinduliwa jijini Arusha.

Mradi huu unashirikisha mashirika matatu ambayo ni Shirika la wanahabari la utetezi wa jamii za pembezoni ( MAIPAC),Taasisi ya Uraia na Msaada wa Kisheria (CILAO) na Shirika la Kusaidia Ustawi wa Wanawake na Watoto (WOCWELS)

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Cilao Odero Charles alisema vyuo vikuu vinavyohusika ni Tumaini Makumira Mtakatifu Agostino Centa ya Arusha na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru-TICD)  pia alisema lengo la mradi huo ni kuwajengea uelewa na ujasiri Wanawake Vijana walioko kwenye Taasisi ya elimu ya juu kuweza kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi

"Tunawataka wanawake vijana waliopo Elimu ya juu kutumia vyema mitandao kwa kupaza sauti dhidi ya ukatili wanaofanyiwa vyuoni" Odero Charles

Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC ,Mussa Juma alisema katika mradi huo, kutakuwa na kampeni katika vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii pia kutakuwa na mafunzo kuhusu Usalama na Ulinzi kwenye Mitandao ya kijamii na kuhakiki usahihi wa taarifa .

''Wasichana mliopo  kwenye Taasisi za elimu ya juu, msiwe wanyonge katika   kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi" alisema juma

Kwa upande wake Mary Mushi Mkurugenzi wa shirika la WOCWELS alisema katika mradi huo kutakuwa na mafunzo kuhusu Sheria na Sera zinazolinda matumizi ya Mitandao nchini

''pia kutakuwa na dahalo kuhusu matumizi ya dijitali  na fursa hivyo tunataka wasichana kwenye Taasisi za elimu ya juu kutumia mitandao vizuri na tutatumia hashtags maisha salama, fursa zaidi na digitali"alisema

Wakizungumza katika uzinduzi huo, viongozi wa serikali za wanafunzi vyuo Cha St Agostini, Makumira na taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru walieleza kuwa watashiriki vyema mradi huo kwani unamanufaa kwao.

Awatif Mshana  waziri wa Afya SAUT Arusha  alisema wanachuo wasichana wamekuwa waoga katika kutumia mitandao kutokana na baadhi ya watu kuitumia kuwadhalilisha.

"Tunaamini elimu hii itakwenda kutuunganisha wanachuo wasichana na kutumia vizuri mitandao"alisema.

Ester Koka mwanafunzi chuo kikuu cha Tumaini Makumira alisema wanasichana wengi chuoni wamekuwa hawatumii vizuri mitandao lakini yeye anatumia vizuri na amenufaika kupata fursa mbalimbali.

Joyce Athanas mwanafunzi chuo Cha Maendeleo ya jamii Tengeru alisema anaimani Kupitia mradi huu atakwenda kutumia mitandao vizuri na kupaza sauti juu ya ukatili vyuoni.

Ruth Usanga mwanafunzi wa SAUT Arusha aliwasilisha wanachuo wenye ulemavu alisema wengi wao wapo vijijini hawajuwi fursa zilizopo kwenye mitandao hivyo atakuwa balozi mzuri kumfikisha elimu vijijini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI