MKOA wa Pwani umetenga kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya kuyakopesha makundi maalumu wakiwemo watu wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa mjini Kibaha na katibu Tawala RAS mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akifungua kongamano kwa viongozi na wanachama wa Chama Cha Wasioona (TLB) wakati wa maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe Kitaifa.
Tumbo amesema kuwa serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona ili waweze kupata fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.
Amesema kuwa wa katika kuona umuhimu wa kiwawezesha watu wenye ulemavu imeweka utaratibu wa kila Halmashauri kutoa asilimia mbili ya mapato yao kwa ya kuwakopesha watu wenye ulemavu.
"Fedha hizo ni mgawanyo kwenye Halmashauri zote za mkoa wetu na fedha hizo zipo ambapo makundi hayo ya wanawake na vijana ambao katika fedha hizo wanakopeshwa kwa asilimia nne na asilimia mbili ni watu wenye ulemavu,"alisema Tumbo.
Aidha amesema kuwa watu wasioona ni miongoni mwa makundi yanayonufaika na fedha hizo ambapo kila Halmashauri inatakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kila mwaka kwa ajili ya kuyakopesha makundi hayo.
Naye mwenyekiti wa TLB Taifa Omary Mpondelo amesema kuwa kongamano hilo ni jukwaa kwa ajili ya wasioona kuelezea na kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi,teknolojia,afya na masuala mengine ya kimaendeleo.
Mpondelo amesema kuwa licha ya kupata mafanikio mbalimbali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mtazamo hasi wa jamii dhidi yao na kuwaona kama watu wasio na uwezo wa kufanya shughuli kama watu wanaoona.
Kwa upande wake Angela Sebastian ambaye ni mjasiriamali amesema kuwa changamoto kubwa ya namna ya kuyafikia masoko kutokana na hali zao.
Mwisho.
0 Comments