Mkwajuni- Songwe
Diwani Kata ya Mkwajuni Shaibath Kapingu amefanya kikao kazi na waalimu, wajumbe wa Bodi,wataalamu wa Kata katika Shule ya Sekondari Sume iliyopo katika Kata ya Mkwajuni.
Kikao hicho kimepokea taarifa na kupongeza serikali kwa kutoa fedha Milioni 150 kwa ajili ya shule ya Sume sekondari ambapo milioni 125 ni kujenga Madarasa Mapya Saba na milion 25 ni kukamilisha maboma mawili na Ofisi yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi.
Aidha kikao hicho kilisisitiza kazi kufanyika kwa viwango na kuhakikisha madarasa yanapokamilika na madawati yanakuwepo kwa mujibu wa muongozo.
Aidha kikao kimeridhia nguvu za Wananchi kutumika kwa kuanza kumwaga mawe lori 10 kwa ajili ya shughuli za ujenzi na pia umwaga mchanga zaidi ya Lori 12 za awali kwa ajili ya ujenzi kazi hizo zote zifanywe na wananchi ili kuongeza thamani ya fedha na kuunga mkono jitihada za serikali na kusisitiza fursa zote ambazo ni nguvu za Wananchi kuanzia kesho zianze kupelekwa shuleni.
Katika hatua nyingine Diwani huyo amewapongeza wajumbe kwa kuhudhuria na kuwaomba kwa dhati kuendelea kuijenga Sume sekondari na ameendelea kuishukuru Halmashauri ya Songwe kupitia Kwa Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi na wananchi wana Imani kubwa sana.
Hata hivo Diwani huyo amewatakia kila mmoja kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake miradi hiyo kukamilika kwa mujibu wa maelekezo ya serikali yaliyotelewa.
0 Comments