Polisi nchini uganda wamethibitisha kwamba takriban watu sita wamefariki katika milipuko iliyotokea mjini Kampala mapema leo.
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha ndani juu ya idadi ya vifo.
NTV Uganda imesema Meya wa Kampala Salim Uhuru ndiye chanzo cha habari za vifo vya watu wawili vilivyoripotiwa hapo awali
Ripota wa NTV alisema aliona sehemu za mwili zikiwa zimetapakaa katika eneo moja la mlipuko huo:CHANZO BBC
0 Comments