Header Ads Widget

MAHAKAMA YATUPA PINGAMIZI LA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA TABORA.

Shauri la Madai linalomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya akitakiwa kulipa Fidia ya  Shilingi Milioni 140 limepangwa kutajwa Novemba 09/2021 baada ya mahakama kutupa pingamizi la mdaiwa. mwandishi wa matukio daima Lucas Raphael anaripoti kutokea Tabora

Akihairisha Shauri hilo hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora Nzige Sigwa alisema hoja zilizowasilishwa na Wakili wa Mdaiwa zikitaka shauri hilo liondolewe hazina mashiko kisheria.

Hakimu Nzige akitoa Maamuzi hayo madogo alisema Mahakama imejiridhisha kwamba wakili wa mdai Kelvin Kayaga alifuata taratibu na Kanuni zinazohusu mashauri ya Madai.

Komanya kupitia kwa Wakili wake Issa Rajabu Mavulla aliwasilisha pingamizi Mahakamani hapo akitaka shauri hilo liondolewe kwa kile alichodai mlalamikaji Alex Ntonge alishindwa kuanisha madai yake kwa mujibu wa sheria.

Wakili Mavula aliiambia Mahakama hiyo kuwa hakuna Madai ya msingi Hivyo mteja wake ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya wa Zamani hawezi kulipa fedha hizo.

Alex Ntonge ambaye ni mdai katika shauri hilo alitaka alipwe shilingi milioni 140 kama fidia kutokana na Kudhalilishwa pamoja na kufunguliwa kesi ya jinai kwa nia hovu.

Wakili Kayaga ambaye anamwakilisha mdai aliiambia  Mbele ya Hakimu

Awali Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora Nzige Sigwa upande wa Mdai ukiongozwa na wakili Kayaga ulidai kwamba mdaiwa alimdhalilisha mteja wake Alex Ntonge  Januari 05/2021.

Aliongeza kuwa siku hiyo mdaiwa Kitwala Komanya ambaye wakati huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askali wa jeshi la Polisi walifika nyumbani kwake na Kumdhalilisha.

 

Kwamba  mdaiwa akiwa na askali wenye Silaha baada ya kufika nyumbani hapo walimkamata mdai Alex Ntonge na kisha walimfanyia vitendo vinavyodhalilisha utu wake mbele ya famiria yake na majirani zake.

 

Mdaiwa katika Shauri hili Kitwala Komanya alienguliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya na Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Saima Suluhu Hassan juni 19/2021 baada ya Kupangua nafasi za wakuu wa Wilaya.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI