Waendesha magari ya abiria Mkoani Kagera wameshauriwa kubadiri route zao pindi wanapogundua kuwa route walizopo kwasasa aziwalipi. mwandishi wa matukio daima Titus Mwombeki anaripoti kutokea Bukoba
Hayo yalisemwa na Afisa Mfawidhi LATRA Kagera Shadrack Malale alipotembelewa na MATUKIO DAIMA leo ofisini kwake na kuwataka waendesha magari ya abiria mkoani kagera kuwa wanaleta maombi yao ofisini hapo wanapopatwa na tatizo kama hilo.
“ Tumefanya vikao vingi na waendesha magari katika mkoa wetu, na kila mara tumekuwa tukiwaomba walete maombi yao ya kubadili routes zao pale wanapogundua kuwa hawapati faida katokana na kuwa kwenye route fulani baadhi wameleta na wamebadilishiwa lakini wengine awaleti wanaishia kunung'unika kitu ambacho sio kizuri” alisema Malale.
Sambamba na hilo afisa huyo alisema kuwa katika mkoa wa Kagera kuna route nyingi hivyo waendesha magari ya abiria wasijifunge kwenye route moja wakati route hiyo aiwanufaiki na route hiyo walete kero zao ziweze kufanyiwa kazi.
“ Sisi hatujamfunga mtu kwamba asibadiri ‘route’ mtu anapoamua kubadiri aje ofisini tuone anapotaka kuamia kuna uwezekano au haiwezekani na baadaya ya hapo tunafikia muafaka kwani lengo letu sisi ni kuona waendesha magari ya abiria wananufaika sio kunung'unika”. alisema
Aliongeza kuwa suala la nauli kutoendana na wakati ni suala la nchi nzima kwani upangaji wa nauli unaotumika kwasasa ulipangwa mwezi wa pili 2013 na sio kwa leo tu bali hata kwa miaka ijayo na utaratibu wa kubadili nauli ukiitajika nchini litafanyiwa kazi lakini sio kwa mkoa bali nchi nzima.
0 Comments