Katibu mpya wa vijana Mkoa wa Mwanza Dennis Nyamlekela amewataka vijana kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kufikia hadhima na malengo ya chama cha mapinduzi yaliyofanya chama hicho kikaaminika katika uchaguzi wa mwaka 2020 yanatekelezeka. mwandishi wa matukio daima Chausiku Said anaripoti kutokea Mwanza
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mapokezi alisema kuwa wamejipanga vizuri na viongozi wenzake kuhakikisha wanatekeleza majukunu yao kama ipaswavyo ili kuweza kufanikisha mipango yote ya Rais Samia kama alivyoelekeza.
Dennis alieleza kuwa kutokana na fedha ambazo Rais amezitoa kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, kutengeneza madawati, pamoja na vituo vya afya hivyo anapaswa kushirikiana na vijana ili kufikia malengo hayo.
" jambo la mama ni letu sisi sote na kila tunalolifanya ni jambo la mama" alisema Dennis
Hata hivyo alieleza kuwa atahakikisha anaendeleza umoja wa vijana pale alipoishia katibu aliyekuwepo kwa kutafuta fursa kwa ajili ya vijana na kuweza kuzifahamu fursa hizo za kiuchumi katika maeneo yao ili kuweza kuwa imara katika kutekeleza majukumu ya chama.
Aliwataka vijana kuchangamkia fursa za ujasiliamali pamoja na fursa zinazotangazwa na serikali katika kushiriki kwenye ujenzi wa madarasa.
"Nitahakikisha nafuatilia na kuwashirikisha kwa kila jambo linaloendelea Katika fursa mbalimbali zinazopatikana" Alisema Dennis.
Aidha alitoa wito kwa vijana kuunga mkono juhudi zote za Rais Samia na kuachana na watu wasio na nia njema na kupotosha jamii.
0 Comments