Header Ads Widget

KAMPUNI YA ETDCO YATENGENEZA FAIDA YA BIL. 9.6

 




Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme (ETDCO) iliyopo chini ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesema hadi kufikia June 30, mwaka huu metengeneza faida Jumla ya shill bill 9.6 tangu kuanzishwa kwake.....Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Kauli hiyo, imetolewa leo na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Mhandisi MacLean Mbonile wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mafanikio ya kampuni hiyo katika  kushereheka miaka 60 ya uhuru.



Amesema kuwa, ETDCO mpaka sasa imetekeleza jumla ya miradi 74 yenye thamani shill bill 156.03  tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 huku miradi 15 yenye thamani ya shill bill 151.48  bado inaendelea kutekelezwa na kampuni hiyo.


Amesema kuwa, miongoni mwa miradi 74 iliyotekelezwa na kampuni hiyo ni pamoja na ujenzi wa njia ya  kusambaza umeme kutoka Morogoro hadi kwenye mradi wa kuzalisha umeme wa bwawa la Julias Nyerere pamoja na Ujenzi wa njia ya kupeleka umeme yenye uwezo wa 33kV kutoka Mahumbika hadi Ruangwa.



Ameongeza kuwa, mradi mwengine ni Ujenzi wa njia ya kupeleka umeme yenye uwezo 33kV kutoka Nanyumbu hadi Tunduru ambapo una thamani ya shill bill 1.5, pamoja na Ujenzi wa njia mbili kutoka Gongolamboto hadi kwenye mradi wa kuzalisha umeme kutoka kwenye bwawa la Julias Nyerere ambapo mradi huo uliingizia kampuni sh bill 17.8.


"Hii ni miongoni mwa miradi mikubwa 74 iliyokwisha kamilika, Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye uwezo wa 132kV kutoka Mtwara hadi Lindi, huu ni mradi mkubwa wa kwanza kutekelezwa na kampuni hii tangu  kuanzishwa kwake"amesema Mbonile.



Ameongeza kuwa, mradi huo ulihusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye umbali wa kilomota 80 kutoka kituo Cha umeme (Substion) ya Mtwara hadi kwenye kituo cha umeme Mahumbika kilichopo Mkoani Lindi.


Vile vile, amesema Ujenzi mwengine ni wa kupeleka umeme kutoka Geita hadi kwenye mgodi waSerikali wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo Wilayani Biharamulo ambao una thamani ya sh bill 6.4 pamoja na Ujenzi wa njia ya kupeleka umeme kwenda mji wa Kiserikali Mtumba na Ikulu Chamwino ambao umegarimu shill bill 3.4, ulikamilika mwaka 2020.



Katika hatua nyengine, amesema mbali na miradi iliyokamika lakini pia kuna miradi mingine 15 inayoendelea,inayogharimu shill bill 151 ukiwemo REA awamu ya ||| mzunguko  wa || mikoa ya mbeya na Katavi ambapo itahusisha kupeleka umeme kwenye Jumla ya vijiji 194 sh bill 64.5 ambapo inatakiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwaka 2022. 


Ameongeza kuwa, mradi mwengine  ni Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wenye uwezo wa 132kV kutoka Tabora kwenda Katavi  na Tabora kwenda Kigoma ambapo itawezesha kufikisha umeme wa gridi ya Taifa kwenye mikoa Katavi na Kigoma, ambapo itahusisha njia zitakazojengwa zenye jumla ya urefu wa kilomita 776, zenye thamani ya sh bill 15.9 miradi hii itakamilika mwishoni mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI