NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro Profesa Patrick Ndakidemi ameishukuru serikali kwa kutoa fedha 1,060,000,000 kwa ajili ya ujenzi madarasa 53 katika shule za sekondari katika jimbo hilo.
Profesa Ndakidemi alisema kuwa, fedha hizo zitamaliza tatizo la uhaba wa madarasa katika shule za sekondari za serikali zilizokuwa na upungufu jimboni huko.
Alisema kuwa, fedha hiyo imetoka katika mfuko wa mpango kabambe wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa dhidi ya Uviko-19.
"Wananchi wa jimbo la Moshi vijijini tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hasani kwa jinsi anavyopambana kuhakikisha anatutetea sisi wananchi wake na kutuletea maendeleo tunaahidi kumuunga mkono kwa kuhakikisha tunasimamia fedha hizi zitumike kama zilivyokusudiwa" alisema Prof. Ndakidemi.
0 Comments