Header Ads Widget

IRINGA KUWA KITUO CHA UTALII KUSINI


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuwa Mkoa wa Iringa uwe kituo cha utalii katika ukanda wa Kusini kwa kuelekeza nguvu nyingi katika vifaa, ujenzi na miundombinu mbalimbali inayohusu vivutio vya utalii. mwandishi wa matukio daima anaripoti kutokea Iringa

Hayo yalisemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa jana tarehe 31 Oktoba wakati akisoma taarifa ya serikali mkoani Iringa na kusema kuwa Tanzania ni Nchi ya pili Duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikitanguliwa na Brazil, hata hivyo vivutio vyetu vimekuwa havitufaishi kwa kiwango kinachotakiwa.

''ndugu zangu waandishi wa habari na watanzania, sote tunatambua kuwa moja ya maeneo yanayochangia fedha nyingi katika pato la taifa letu ni utalii, unachangia kwa asilimia 17.2, unaajiri watu milioni 1.6 na unachangia fedha za kigeni kwa asilimia 25, na yapo maeneo mengi ambayo kuna vivutio vingi vya utalii lakini havitunufaishi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokufunguliwa kwa miundombinu ya kuvifikia na kutokuwepo kwa huduma kwa watalii hivyo serikali imeamua kuja na mradi uitwao REGROW'' alisema 

Gerson alisema kuwa tayari Serikali ishatenga shilingi bilioni 345 kwa ajili ya kujenga miundombinu, magari 44, mitambo pamoja na ujenzi wa kituo cha pamoja cha masuala ya utalii(One Stop Center).

''fedha hizo ni kwa ajili ya kujenga barabara kilometa 2,000, majengo zaidi ya 80, viwanja vya ndege vya hifadhini 14, usimamizi wa mradi huduma za utalii,  magari 44 kwa ajili ya doria pamoja mitambo 16 ya kutengenezea miundombinu ndani ya hifadhi yameshanunuliwana kazi imeshaanza, pia kuna mkandarasi yupo kazini katika skimu ya Madibila anaendelea na kazi ya kuboresha miundombinu ya mradi huu,''.

Hata hivyo alisema jengo la One Stop Center litajengwa maeneo ya Kihesa Kilolo kuanzia Juni mwaka 2022 kwa gharama ya shilingi bilioni 16 na milioni 590 lengo ni kiwe kituo cha kisasa ambacho kitahudumia ukanda wote wa kusini ambapo itasaidia kuongeza idadi ya watalii pia pato la taifa litaongezeka.

Kupitia mradi huu Serikali imeamua kuimarisha miundombinu na huduma za utalii katika hifadhi za Taifa Ruaha, Nyerere, Mikumi na Udzungwa ambayo yana kilometa za mraba 56,339 ambapo utagusa mikoa ya Iringa, Pwani, Mbeya ,Dodoma, Njombe na Morogoro pia kuna vijiji 61 katika wilaya ya Kilolo, Iringa Vijijini, Rufiji, Kisarawe, Chamwino, Morogoro Vijijini, Mbarali, Kilombero, Kilosa na Mvomero ambavyo vitanufaika na mradi huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI