Header Ads Widget

HALMASHAURI YA WILAYA YA UYUI YATUMA BARUA YA PONGEZI KWA RAIS SAMIA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui imetuma barua ya pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia  kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba 123 vya madarasa kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya UVIKO 19 . mwandishi wa matukio Lucas Raphael anaripoti kutokea Tabora

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya wenzake aliikabidhi barua hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani kwa ajili ya kumfikishia Rais Samia.

Alisema kwa kipindi kifupi cha uongozi wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia , Uyui imepata fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 2.4 ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Sekondari na bilioni 1.1 kwa ajili ya vyumba vya madarasa katika Shule Shikizi.

Ntahondi alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 90 ni za  ujenzi wa watumishi  wa sekta ya afya na milioni 14.1 kwa ajili ya fedha za ufuatiliaji.

Alisema watahakikisha wanatumia kiasi cha milioni 20 kukamilisha darasa moja kama walivyoekelezwa na kiasi kingine kibaki .

Ntahondi aliongeza hivi  Madiwani na Watendaji wa Halmashauri hiyo wamejipanga kusimamia ili kuhakikisha fedha zinatumika kwa makusudio yaliyopangwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI