Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watuhumiwa wanatakiwa kuheshimiwa na kutendewa haki kama watu wasio na hatia mpaka itakapobainika vinginevyo.
IGP Sirro alitoa kauli hiyo jana, wakati akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women) pamoja na Mtandao wa polisi wanawake ndani ya jeshi hilo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (TPS).
Mafunzo hayo yalienda sambamba na uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo wa namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.
“Hakuna kitu muhimu kwetu kama kusimamia sheria na kutenda haki, kuwa wanyenyekevu na kuheshimu watu. Sisi leo tumevaa majoho haya na kesho tunarudisha kwa wenyewe na wenyewe ni Watanzania ambao wanalipa kodi ambayo inatufanya tufanye kazi.
Pamoja na mambo mengine, alisema zipo jitihada za utatuzi wa changamoto mbalimbali ndani ya jeshi hilo, ikiwamo masuala ya utumishi .
“Nitajitahidi katika upangaji wa nafasi za utendaji kazi kwa maofisa wanaondelea na mafunzo vyuoni wanaomaliza hivi karibuni ili madawati haya ya jinsia yaweze kupata uwakilishi kuanzia ngazi za vituo, wilaya hadi mkoa,” alisema.:chanzo Mwananchi
0 Comments