Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wananchi wameombwa kujitokeza na kushiriki katika shughuli za kijamii hali ambayo itachangia tija na ufanisi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo .
Rai hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole wakati akishiriki kwenye shughuli ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Mwasele .
Diwani Mwendapole amewaomba wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi pale kunapotokea tangazo muhimu linalowalenga ili kuimarisha ushirikiano
“Nawaomba wananchi wa kata ya Kambarage kujitokeza kwa wingi kwenye masuala ya maendeleo kadri tunavyotangaziana tujitokeze kwa wingi na kuwa na moyo wa kujitolea”
Alisema kuwa Kukamilika kwa madarasa kutasaidia wanafunzi kukaa kwa nafasi katika madarasa na hakutakuwa na mbanano mkubwa kwa wanafunzi .
Huku diwani wa viti maalum Manispaa ya Shinyanga Sheilla Mshandete ameipongeza serikali kwa mpango wa ujenzi wa vyumba vya madarasa hatua ambayo itasaidia kuongeza ari ya wanafunzi kujisomea.
“Kwanza kabisa tunampongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa tunaamini kabisa mwakani hakuna mtoto atakaye kosa darasa watoto wetu wote wataingia madarasani tumeuona mfano kwa kipindi kifupi tu cha mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan madarasa yanajengwa kwa kasi nchi nzima ikiwemo kata yetu ya Kambarage katika shule yetu ya Mwasele leo tunafukio msingi wetu kwa ajili ya kunyanyua madarasa na tunategemea kufika mwezi wa kuminamoja taerehe 15 darasa litakuwa limesimama na tayari tunamalizia sehemu za kawaida ili watoto watakapo kuja wakute madarasa yako tayari”
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Kambarage Adella Mukinga amesema kukamilika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo itaondoa changamoto ya upungufu wa madarasa
“Katika mpango wetu wa kujenga madarasa sekondari kwa mwaka huu tulikuwa na mpango wa kujenga vyumba vya madarasa 6 mwanzo tulianza kujenga vyumba viwili kwa nguvu ya wananchi serikali mwezi wa sita ilituongezea vyumba viwili na sasa tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea tena ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika vipaumbele vyetu vya kujenga vyumba vya madarasa sita mwaka huu tumevikamilisha kwahiyo kama vyumba vipo watoto watasoma bila kuwa na mashaka kwamba watasomea wapi na watakaa wapi”
Akizungumza makamu mkuu wa shule ya sekondari Mwasele mwalimu Baraka Russewa amesema serikali imewapatia kiasi cha fedha milioni 40 ambapo amesema jumla ya wanafunzi wa shule hiyo 749 huku akiwakumbusha wanafunzi kujipanga kusoma kwa bidii ili kuongeza ufaulu“
Wanafunzi wajipange wasome kwa bidii serikali imesema elimu ni bila malipo kwahiyo wao waongeze nguvu yao kwenye kusoma waache michezo wazingatie muda wao na wanapokuwa nyumbani wawasikilize wazazi na walezi wao itasaidia kupandisha taaluma yao”
0 Comments