Header Ads Widget

HABARI PICHA; Rais Samia Suluhu Hassan azungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Lord Walney, Glasgow, Scotland

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Mhe Rais Samia ameshawasili Glasgow kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney mara baada ya kuzungumza naye katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. Wengine katika picha wa kwanza (Kushoto) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberatha Mulamula na wa kwanza (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza katika masuala ya Biashara Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshugulikia masuala ya Biashara kati ya Tanzania na Uingereza Mhe. Lord Walney wa kwanza kulia katika mji wa Glasgow, Scotland leo tarehe 31 Oktoba, 2021. PICHA NA IKULU

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI