MATUKIO MBALIMBALI WAKATI DKT. NCHEMBA(MB), AKIZUNGUMZA KUHUSU MAFANIKIO YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KATIKA YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, ambapo ametoa rai kwa Watanzania wote kushiriki katika zoezi sensa ya watu na makazi mwaka 2022, ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa ufanisi, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mawasiliano Serikalini, Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa, akizungumza wakati akihitimisha mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango . Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Hayumo pichani,) na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha ya katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, jijini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiandika maswali ya waandishi wa Habari wakati wa mkutano na vyombo vya Habari kuhusu mafanikio na changamoto za Wizara yake katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Hayumo pichani),
0 Comments