Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe, Joseph Mkude ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kutekeleza takwa la kisheria kuvikopesha vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu shilingi milioni 143 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mhe, Mkude alisema hayo alipokuwa akiongea na wananchi wa Kishapu waliojitokeza katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kabla ya tukio la kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 143 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
"Niwashukuru na kuwapongeza sana kamati ya fedha uchumi na mipango chini ya mwenyekiti wa Halmashauri Mhe, William Jijimya. Pongezi hizi ziwafikie pia watendaji wote wakiwa chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Emmanuel Johnson kwa kutekekeleza kikamilifu maelekezo ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Mhe, Samia Suluhu Hassan. Hongereni sana Kishapu na tutazidi kuneemeka kuna mazuri mengi yanazidi kumiminika Kishapu yetu." Mhe Mkude alisema.
Aidha Mkuu wa wilaya aliitaka Halmashauri kuendelea kutoa mikopo mikubwa kwa vikundi na kudhidi kuwaelimisha manufaa ya kuwa na vikundi kwa sababu vinaongeza tija kwa wananchi.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kiashapu Dr Sabinus Chaula alisema kuwa kwa kipindi cha robo ya kwanza
2021/2022 jumla ya shilingi milioni 143 zimekopesha kwa vikundi 37 alisema vikundi vya Wanawake 21, Vijana 14 na watu wenye ulemavu wawili.
0 Comments