Jumla ya vijana 48 kutoka katika vijiji vya Michenga A na B Katika kata ya Malolo halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi leo tarehe 5 Novemba wamehitimu mafunzo ya jeshi la Akiba huku 24 wakishindwa kuhitimu mafumzo hayo. mwandishi wa matukio daima Hadija Omary anaripoti kutokea Lindi
Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma Alimuagiza Katibu tawala wa Wilaya hiyo pamoja na mkurugezi wa halmashauri ya Ruangwa kuhakikisha shughuli zote zinazohitaji kutumia walizi na wasimamizi wa Amani kuwatumia vijana waliohitimu mafunzo hayo.
Ngoma alisema pamoja na kutambua kazi kubwa iliyofanywa na vijana hawa lakini Pia rasilimali za Nchi zimetumika kwa muda wote wa zaidi ya miezi mitatu ambayo vijana hao wakiwa wanapatiwa mafunzo hayo.
"Sitopenda kusikia kwamba tumeenda kuokota watu mitaani wakati tunao vijana walioiva na wamekula kiapo cha kutetea Taifa lao na katika hili naahidi kufuatilia na kuhakikisha mazoezi yote yanayohitaji makamanda vijana hawa wanatumika"
"Kazi hii ambayo imefanywa na vijana hawa kwa wale ambao hawajawahi kupita kwenye maeneo haya ya kiu za kijeshi unaweza kuiona kama ni kazi nyepesi na yakawaida lakini tukikuzungusha ndani ya Dakika mbili unaweza kutoa ulimi nje." alisema
Pamoja na mambo mengine Ngoma pia Alitoa wito kwa wananchi wa vijiji hivyo kutoa ushirikiano kwa vijana hao pindi watakapoanza utekelezaji wa majukumu yao huku akiwataka vijana waliohitimu mafunzo hayo kulinda kiapo cha jeshi kwa kuitetea Nchi pamoja na kulinda amani ya Nchi yao
Kwa upande wake mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ruangwa Meja Burure Magige, Alitaja sababu za vijana hao 24 kushindwa kuhitimu mafunzo hayo ni Afya , utoro pamoja na nidhamu ambapo mienendo na tabia zao hazikulidhisha hivyo ikawafanya kushindwa kumaliza.
Pia Meja Magige alieleza kuwa vijana hao waliohitimu mafunzo hayo wameweza kujifunza mambo mbali mbali ikiwa pamoja na mafunzo ya kijeshi, stadi za kazi, mbinu za kivita, ujanja wa polini, masuala ya uokoaji, uhamiaji na usalama wa Barabarani
Onesmo Chitawala ni mtemdaji wa kijiji cha michenga A na muhitimu wa Mafunzo hayo ya jeshi la Akiba alisema kuwa mafunzo hayo yataweza kumsaidia kuongeza ufanisi katika shughuli zake za utendaji kila siku kwa kumuongezea ukakamavu na utimamu wa mwili
Nae Asia swalehe aliwataka wanawake wenzie wenye dhana potofu kuwa 'kuingia kwenye mafunzo ya kijeshi ni mateso' waache na badala yake alitoa wito kwa wanawake kushiriki katika mafunzo hayo ya jeshi la Akiba pindi nafasi za mafunzo hayo zinapotangazwa kwani yanakujenga kuwa mzalendo wa kuipenda nchi yako.
0 Comments