Header Ads Widget

WIZARA YA KILIMO KUJENGA OFISI ZA MAAFISA KILIMO KILA KATA NCHINI

 


Na Rehema Abraham, Kilimanjaro

Wizara ya kilimo  inaendelea kuboresha ofisi za maafisa ugani kwa kuiwekea miundombinu ya thamani za ofisi, tehama ili maafisa ugani wakutane kwa pamoja na wataalamu na watafiti  kujadili Mambo mbalimbali ya jinsi ya kuboresha kilimo hapa nchini.


Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi msaidizi huduma za ugani na utafiti Wizara ya kilimo Charles Mjema wakati akiongea na mafisa ugani katika maonesho ya siku ya chakula yanayoendea katika  viwanja vya pasua  mkoani Kilimanjaro.


Aidha amesema kuwa  vituo hivyo vimeanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma za ushauri wa kilimo mifugo karibu na wakulima ili waweze kukutana ngazi ya kata .


"Kama mnavyofahamu maafisa ugani  wengi hawana ofisi Kama walivyo wenzetu waalimu ,madaktari,Sasa mkulima  akitoka nyumbani anaanza kuwaza aende wapi akampate afisa kilimo ampe ushauri ,kwa hiyo vituo hivi kwanza vimeanzishwa Kama ofisi na tunalenga kwamba maafisa ugani wote ngazi ya kata wawe na ofisi moja "Alisema Mjema.


Sambamba na hayo ameendelea kusema kuwa maafisa ugani hao watakapo Kaa sehemu moja kwa ngazi ya kata ni rahisi kuwahudumia wakulima kwa njia mbili ya wakulima kuja ofisini kupata ushauri na wao wenyewe kwenda shambani kutafuta ushauri .


"Wakulima wengi wamejiunga katika vikundi mbalimbali (tunaita mitandao ya wakulima) wengine ni wajasiriamali ,vikundi vya kuchakata mazao ,vikundi vya kuzalisha mazao ,kwa hiyo vikundi vipo vya aina mbalimbali Sasa vile vituo vya kata vitaakuwa ni sehemu ya kukutanisha vikundi hivyo "Alisema.


Katika hatua nyingine amesema kuwa vituo hivyo kwa sasa vipo takribani 289  katika kata mbalimbali nchi nzima ambapo vinatakiwa kiwepo shamba darasa la kujifunzia wakulima kwani wakulima wanavyofanya kwa vitendo ni rahisi kuelewa na wao kwenda kufanya kwenye maeneo Yao.



Kwa upande wake Zakaria Gadie afisa ugani kutoka Wizara ya kilimo ,idara ya mafunzo huduma za ugani na utafiti amsema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima ya juu ya matumizi ya mtandao wa (mobile kilimo)M _kilimo ambalo ni jukwaa la mawasiliano linalounganisha wakulima, wafugaji ,wavuvi, wafanyabiashara, kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kwa kutumia simu ya mkononi .


"Huu mfumo wa m Kilimo ulianza mwaka Jana na ulizinduliwa na aliyekuwa waziri waziri wa kilimo wakati huo ,na bàada ya uzinduzi tulifanya majaribio katika baadhi ya halmashauri tatu za mkoa wa dodoma ambazo ni halmashauri za chamwino ,kongwa, bahi na soko la kibaigwa bàada ya hapo tuliendelea kusambaza technologia hii kwa Tanzania "Alisema Gadie.


Amesema kuwa kwa sasa mfumo huo umeweza kusajili zaidi ya wakulima takribani milioni Tano mia moja na thelasini na nne mpaka Sasa lakini pia maafisa ugani waliosajiliwa kwenye mfomo huo ni Elfu sita mia tisa themanini na sita .


Hata hivyo amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa m_Kilimo ni kutokana na kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa maafisa ugani Nchini na mahitaji halisi ni Elfu ishirini mia tano thelathini na nane na kuwa na upungufu wa maafisa ugani elfu kumi na tatu na kusema ndio maana mfumo huo umeanzishwa ili kurahisisha mawasiliano kati ya maafisa ugani na wakulima.


"Lengo lingine la kuanzishwa kwa m_kilimo ni kurahisisha  mkulima kupata masoko  na kupitia mfumo huu mkulima ambaye amejisajili katika mfumo wetu anakuwa na uwezo wa kuuliza bei ya mazao kabla hajauza,"Alisema Gadio.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI