WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto imekutana na sekta binafsi na mashirika ya kidini kujadili fursa ya uwekezaji katika sekta ya Afya hasa katika masuala ya vifaa tiba na viwanda vya madawa. mwandishi wa matukio daima Hamida Ramadhani anaripoti kutokea Dodoma
Akizungumza leo jijini hapa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Profesa Abeli Makubi alisema kuwa licha ya kuwa wizara inashughulika na masuala ya tiba lakini pia sekta hiyo ni eneo muhimu katika uwekezaji hivyo wamekutana na wadau hao kujadili jinsia gani wanaweza kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa pamoja kuleta maendeleo katika masuala ya tiba.
"Wafanyabishara na wawekezaji binafsi bado mna fursa nyingi ya kuwekeza kwenye sekta ya afya kuliko kuiachia Serikali peke ake, pia sasa hivi tumeanza kutengeneza chanjo yetu dhidi ya uviko 19 kwa kushirikiana na sekta na tupo makini kwenye hili endapo tutafanikiwa kwenye chanjo tutakua tumefanikiwa kwenye sekta binafsi "alisema Profesa Makubi
Aidha Katibu Mkuu huyo Alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi kwani imekuwa ikisaidia serikali katika kuhamasisha wananchi kuendelea kujikinga na Uviko 19 hasa katika suala la chanjo ya Uviko 19.
"Niwaombe sekta binafsi kuwekeza pia kwenye vyuo vya sekta ya afya kwani bado watanzania wengi wangependa kusomea masuala ya afya hapa nchini,Tanzania ina maeneo mazuri pia ni mahala salama kwa kuwekeza kwahiyo ni fursa kubwa kwa sekta binafsi kuwekeza hususan kwenye sekta ya afya "
Naye Dkt Gina Francis Makwabe Mwenyekiti wa Chama Cha Hospitali na vituo binafsi Tanzania, aliishukuru wizara kuitisha mkutano huo na kuonesha juhudi kuwa Wizara inashirikiana vizuri na sekta binafsi huku akibainisha kuwa Sekta binafsi zimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika uwekezaji kwenye masuala ya Afya nchini hasa katika vifaa tiba na viwanda.
Hata hivyo kwa upande wake Sachi Katwaza mwenyekiti wa Tanzania Asosiation of Famercitical lndustry, waingizaji wa Dawa na vifaaa tiba nchini ameiomba Serikali kuangalia sheria upya hasa ya ulipaji wa VAT Kwa baadhi ya vifaaa tiba vinapowasili bandari na kubainisha kuwa kupingana kwa TIC na TRA kunachangia pia wao kuwa na vikwazo vingi.
0 Comments