WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu ,bunge vijana Ajira na watu wenye ulemavu Jenista Muhagama, amesema jumla ya wafanyakazi Elfu 18300 wa serikali na Taasisi mbalimbali wamehamia dodoma kuanzia juni 2016 hadi juni 2021 huku akibainisha kuwa kiasi cha shilingi bilion 9 zimeokolewa serikalini baada ya serikali kuhamia Dodoma katika majengo ya ofisi zao.Na Hamida Ramadhan MDTV Dodoma
Waziri Muhagama amesema hayo jiji Dodoma wakati akizindua ujenzi wa awamu ya pili wa Ofisi ya Waziri Mkuu
unaotarajia kufanyika katika mji wa serikali utakaogharimu jumla ya shilingi Bilion 42.7 na utakamilika kwa muda wa miezi 16.
"Hapa naomba niseme kitu Uendelezaji uzingatiwe mpongokazi maalumu ulikuwa unasema mradi utamalizika kwa muda wa miaka 2 lakini sisi tunasema mradi huu utamalizika kwa muda wa miezi 16 lazima Ofisi ya waziri Mkuu tuwewakwanza kukamilisha miradi hii," Amesema Mhagama.
Aidha, Waziri Muhagama amefafanua kuwa ujenzi huo wa awamu ya pili utajengwa majengo mawili ya ghorofa sita hadi 11 ambapo katika jengo la sera uratibu na bunge zimetengwa shilingi bilioni 23.5 na jengo la ajira Vijana na kazi zimetengwa bilion 19.2.huku bilioni 300 zikitengwa kwa ajili ya wizara zote 24 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
"Wananchi wa Dodoma na watanzania wote wa mkoa wa Dodoma tunasema Dodoma kumekucha bilioni hizo zinakwenda kufanyakazi Dodoma sasa Vijana jitokezeni kupata ajira kwenye shughuli hizi ," amesema Uhagama
Naye katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tixon Zunda amesema wamefanya upimaji wa udongo lengo likiwa ni kufanya tafiti za kina kwenye miamba ambapo pameonyesha eneo hilo lipo salama kwa ujenzi wa jengo la ghorofa 6 hadi 11.
"Miradi itakamilika kwa muda wa miezi 16 na tumeshaunda kamati ya ufuatiliaji ambayo itakuwa inafuatilia miradi hiyo kwa kushirikiana na mshauri elekezi," amesema Katibu Zunda.
0 Comments