Na, Titus Mwombeki-BUKOBA.
Watu wenye ulemavu mkoani kagera waanza mazoezi ya kuupanda mlima Kilimanjaro zoezi linalotegemewa kufanyika tarehe 29/10/2021.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa shirikisho la vyama vyenye watu wenye ulemeavu mkoani humo ndugu Novati Joseph Mwijage alipotembelea ofisi ya Umoja wa waandishi wa habari KAGERA PRESS CLUB na kusema kuwa zoezi hilo inaambatana na kampeini maalumu ya kutafuta vifaa saidizi kwaajiri ya watu wenye ulemavu mkoani humo.
“Mimi binafsi nishaanza mazoezi ya kuupanda mlima kilimanjalo lakini zoezi hili linaambatana na kampeini maalumu ya kuomba usaidizi wa vifaa kutoka katika makampuni, wadau pamoja na serikali ili kusaidia watu wenye ulemavu mkoani kagera”. Amesema Mwijage.
Sambamba na hilo, amesema kuwa vifaa vinavyohitajika ili kuwasaidi watu hao vinatofautiana kulingana na makundi yao kwani kuna makundi mbalimbali ya walemavu katika shirikisho lao.
“ Tuna makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu hivyo na vifaa tunavyoomba vinatofautiana kulingana na makundi yetu mfano kuna uitaji wa vimbo na magongo kwa watu wenye ulemavu wa viungo, mafuta kofia na miwani ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na fimbo maalumu kwaajiri ya watu wasioona”.
Amehitimisha kwa kusema kuwa, anamewaalika watu wenye ulemavu mkoani humo wanaowiwa na walio tayari kupanda kuupanda mlima Kilimanjaro kujitokeza ili kuweza kupanda mlima huo kwa pamoja.





0 Comments