Header Ads Widget

UCSAF WATAKIWA KUHAKIKISHA WATU WENYE ULEMAVU WANAPEWA KIPAUMBELE MAFUNZO YA TEHAMA




 Na Doreen Aloyce, Dodoma.


WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali ametoa wito kwa mfuko wa mawasiliano kwa wote nchini(UCSAF) kuhakikisha  watu wenye ulemavu wanapewa kipaumbele kwenye mafunzo ya Tehama ili waweze kunufaika na huduma hiyo . 


Ameyasema hayo jijini Dodoma alipotembelea ofisi za UCSAF ambapo amesisitiza huduma za mawasiliano hazipaswi kuwaacha nyuma watu wenye ulemavu kwani nao wanahaki ya kunufaika na huduma hizo.


"Tunapoenda mbele zaidi Katika Mawasiliano hatupaswi kuwaacha wenzetu hawa watu wenye Ulemavu kwani wakipatiwa  mafunzo watakuwa na uelewa zaidi"amesema Waziri Rahma


Aidha Waziri huyo amesema kuwa Katika  kisiwa cha Pemba wananchi wake bado wana changamoto ya mawasiliano hivyo wanapaswa kutatuliwa kero zao.



"Kisiwa kile Kwa upande wa Mawasiliano Bado hakijawa vizuri kwahiyo ninyi UCSAF kwavile ni mfuko wa Mawasiliano fanyeni jambo  kwa maana awali nilikuwa sijauelewa  mfuko huu ila kwa Leo nmeweza kuufahamu "amesema Rahma


Kwa upande wake mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF  Justina Mashiba ameelezea  hatua wanazoendelea kuzichukua ili kuhakikisha huduma ya mawasiliano zinawafikia wananchi wote wa Zanzibar. 


"Mfuko unaendelea kupambana ili kuweza kuhakikisha huduma ya mawasiliano inapatikana kote,na lengo ni Kila sehemu kuwe na Mawasiliano" amesema Mashiba.

 

Hata hivyo pamoja na Waziri huyo kutembelea mfuko huo pia amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa  jengo la Ofisi ya mfuko huo wa UCSAF linalojengwa Katika eneo la njedengwa Jijini hapa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI