Header Ads Widget

WALENGWA WA TASSAF WAIPONGEZA SERIKALI KUANZISHA MFUMO WA KIELETRONIKI KWENYE MALIPO YAO

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF) waliopo kwenye Mpango wa Kunusuru kaya Masikini awamu ya  Tatu mzunguko wa pili katika kata ya Kiwalala halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi  wameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki ambao unalenga kuwalipa walengwa hao kimtandao. mwandishi wa matukio daima Hadija Omary akiripoti kutokea Lindi.

Wakizungumza na Matukio Daima wakati wa zoezi la kupata taarifa za walengwa hao ili kubadili mfumo wa kupata fedha kutoka Mkononi kwenda kieletroniki walengwa hao wamesema wanaipongeza serikali kwa kubuni mfumo huo kwani utajenga uaminifu kwa watendaji wanaohusika kutoa fedha hizo kwa walenga.

Kwa upande wake Fatuma Nampenda alisema kuwa kwa mfumo unaotumika sasa umekuwa na kasoro nyingi ikiwepo ya utofauti wa malipo kila wataalamu hao wanapokwenda  kufanya malipo kwa walengwa kunakotokana na malipo hayo kufanywa  Mkono kwa mkono

" serikali imefanya vizuri kwa mtazamo huu bora haya kuliko yale ya kwenda Mkono kwa mkono maana mule ndo tunakuwa tunachinjwa kwa sababu leo hii mimi kama nilikuwa napokea Elfu 38000 siku nyingine utakuta napokea Elfu 32000 je hela hii nyingine inakwenda wapi?

Nae Tabu Mathayo Alisema zoezi hilo amelipokea vizuri kwa kuwa sasa hatalazimika kukaa ofisi za kata ama kijiji kwa muda mrefu kwa ajili ya kusubiri malipo kwani hali hili ilikuwa inapelekea baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazopaswa kufanywa na walengwa hao kusimama

"Kwangu mimi zoezi hili nimelipokea na nimelifurahia kwa sababu linaraisisha  kwa kuingiziwa hela kwenye simu hivyo nafanya kazi zangu kwa wakati, sitoweza kukaa tena ofisini kutwa mzima nikisubiri hela. Nitafanya kazi zangu nitakwenda mara moja sehemu ambayo imepangwa kupokelea hela nitapokea na kuondoka" alifafanua Tabu

Kwa mujibu wa mwezeshaji wa Tasaf Ngazi ya Wilaya Jafarani Mohamed   amesema mfumo huo utahusisha malipo kupitia namba za NIDA,  namba za simu ambazo zimesajiliwa majina sawa na yale waliyojiandikisha kwenye malipo ya walengwa pamoja na akounti zao za kibenk,  ambapo kwa wale wa namba za  NIDA  Wataenda kupokelea pesa katika maeneo yatakayopangwa ambapo mlengwa atahakikiwa kwa kutumia Dole gumba lake

Aliongeza kuwa kwa wale  watakaoandikisha namba za Simu watapokea pesa kwenye simu zao na wale walioandikisha namba za Bank watapata fedha kupitia kwenye ankaunti hizo.



Alisema lengo la mfumo huo ni kuwapunguzia adha walengwa kukaa muda mrefu wakisubiri malipo pamoja na kuwafanya wawe na nidhamu ya matumizi ya fedha zao pamoja na usalama wa fedha hizo

"Muda, tunaweza kuwaahidi walengwa kuwa tutafika saa nne ama saa tano lakini kutokana na changamoto za kibenk usafiri na mambo mbali mbali inaweza ikafika hata saa saba ndo tunafika pale kwa ajili ya kufanya malipo lakini kwa mfumo huu hawatasubiri tena bali utamfanya mlengwa baada ya kusajiliwa tangazo la malipo litatoka ambapo mlengwa ataenda kwa mtu maalumu ambae amewekwa na kuchukuwa pesa yake na kuondoka bila kusubiri tena " alifafanua Jafarani

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI